Watu 10 wameripotiwa kupoteza maisha kwenye shambulizi la bomu lililotekelezwa katika kituo cha elimu cha Kawthar kilichoko katika mji mkuu wa Kabul nchini Afganistan.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani Tarık Aryan, alitoa maelezo na kufahamisha kutekelezwa kwa shambulizi la bomu kwenye kituo cha elimu cha Kawthar katika eneo la Dasht-i Barji.
Aryan alibainisha kuuawa kwa watu 10, na kujeruhiwa kwa watu wengine 20 kwenye shambulizi hilo kwa mujibu wa taarifa za awali.
Mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa idadi ya vifo ilikuwa nyingi zaidi na shambulizi lilikuwa ni la kujitoa mhanga.
Hakuna yeyote aliyehusishwa na shambulizi hilo.