STAA wa filamu za Bongo Muvi, Shamsa Ford amefarijiana na staa mwenziye ambaye ni mjasiriamali, Faiza Ally kuwa kutendwa na wanaume ambao wamezaa nao kumewafanya wakawa wanawake wenye maendeleo na ndoto kubwa sana.
Akizungumza na Amani, Shamsa alisema kuwa yeye na Faiza wakizungumza wanaweza kusikilizana sana kwa sababu wamepitia machungu ya kulea wao watoto wenyewe tena kwa shida lakini wamesimama.
“Mwanamke yeyote ambaye amepitia matatizo ya kulea mtoto mwenyewe anaweza kujua nazungumza nini na ndivyo ilivyokuwa kwa mimi na Faiza, tunaweza tukazungumza lugha moja na tukaelewana na pia ni watu tunaofarijiana sana kwa kweli na tutatoboa tu tukiwa wenyewe hivihivi bila mwanaume pembeni yetu,” alisema Shamsa ambaye analea mtoto wake Terry mwenyewe bila baba.
Kwa upande wa Faiza alisema kuwa anapenda siku zote kumchukulia mfano Shamsa kwa sababu amepitia hali hiyo na mpaka sasa anapitia lakini hatetereki.
“Tukiwa na kitu chochote kigumu kinatukabili mimi na Shamsa, tunaangaliana na kujiona ni wanawake wa tofauti sana na pamoja na changamoto zetu tunasonga mbele siku zote,” alisema Faiza ambaye pia ni mzazi mwenziye na mgombea ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.