Simba Yaomba Msamaha Baada ya Kuchezeshwa Gwaride Dakika 180

 


 BAADA ya kuchezeshwa pira gwaride ndani ya dakika 180 kwa msimu wa 2020/21 kwenye Ligi Kuu Bara na kuyeyusha pointi sita ilizokuwa inasaka Klabu ya Simba imeomba msamaha kwa mashabiki wao kutokana na kupitia mapito hayo magumu.



Simba ambao ni mabingwa watetezi walianza kupoteza mchezo wa kwanza Oktoba 22 kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Nelson Mandela na walipoteza pia mchezo wa pili Oktoba 26 kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru.


Nahodha wa Simba, John Bocco amesema kuwa kutokana na matokeo hayo ambayo wameyapata kwenye michezo miwili mfululizo wanahitaji msamaha kwa kuwa waliteleza na kuahidi kurejea kwenye ubora katika mechi zao zijazo.


"Kwa niaba ya wachezaji tunaomba mtusamehe kwa matokeo tuliyoyapata ya michezo miwili iliyopita tuliteleza na tumeshateleza hatupaswi kuteleza tena.




"Ahadi yetu kwetu kurekebisha makosa yetu na kurudi kwenye sura ya upambanaji mpya kwa michezo yetu ijayo," amesema.




Simba ipo nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 13, imecheza mechi saba na kupoteza jumla ya pointi nane kwa kuwa imelazimisha sare moja na kushinda mechi mbili.




Kinara ni Azam FC mwenye pointi 21 baada ya kucheza mechi nane ameshinda saba na kupoteza mechi moja anafuatiwa na Yanga nafasi ya tatu, pointi 19 amecheza mechi saba na ameshinda sita huku akiwa amelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad