Mgombea Ubunge Jimbo la Mbeya Mjini kupitia CHADEMA, Joseph Mbilinyi amewaomba Viongozi wa Dini wawaombe waumini wachague Wagombea wa Chama hicho, ili waweze kutoa sadaka kwenye nyumba za ibada
Sugu amesema maisha ni magumu na sadaka zimepungua Makanisani kwa kuwa waumini hawana fedha, hivyo kusababisha Viongozi wa Dini nao kuishi maisha magumu
Amesema, “Viongozi wa Dini sio tu mtuombee kwa Mungu ili tushinde Oktoba 28 bali pia, mtuombee kura kwa waumini wenu kwa sababu Serikali ya CHADEMA ina sera nzuri za uchumi zinazokwenda kurudisha kipato kwenye mifuko ya waumini wenu ili sadaka ziongezeke"
-
Aidha, amewataka wananchi waliojiandikisha kupiga kura wasikubali kurubuniwa na watu wanaopita majumbani kuulizia vitambulisho.