BARAZA la Sanaa Tanzania (BASATA) limekanusha taarifa zilizotolewa na Meneja wa mwanamuziki Lady Jaydee (Jide) kwamba limeufungia wimbo wake wa ‘ONE TIME’.
Taarifa iliyotolewa na baraza hilo imesema habari hizo si za kweli na kwamba baraza hilo lilimuita msanii huyo na kufanya naye kikao na kumpa maelekezo ya kufanya maboresho ya wimbo husika na kuuwasilisha ili uweze kupelekwa kwa walaji.