Usipime Aisee...Tigo yazindua Simu Mpya ya TECNO T-Smart 4G

Meneja wa Vifaa kutoka Tigo Tanzania, Mkumbo Myonga akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa simu mpya ya Tecno Tsmart 4G .Pembeni yake anayeshuhudia ni  Woinde Shisael- Meneja Mawasiliano Tigo.

“Simu hii muafaka kwa wateja wote hasa ambao hawajaunganishwa na huduma ya internet” Woinde Shisael- Meneja Mawasiliano Tigo.
#Uzinduzi
#TecnoSmart4G

Dar es Salaam; 13 Oktoba 2020: Kampuni ya mawasiliano inayoongoza nchini kwa kutoa huduma bora za mawasiliano, Tigo Tanzania, leo imetambulisha simu mpya katika soko la simu za mkononi nchini, TECNO T-Smart 4G. Simu hii mpya na ya kisasa itasaidia kuongeza idadi ya watumiaji wa huduma za kidijitali nchini.

Meneja wa Vifaa kutoka Tigo Tanzania, Mkumbo Myonga, amesema, “TECNO T-Smart 4G ambayo hujulikana sana kama TECNO Kitochi itawapa wateja wetu namna bora ya kutumia huduma za kimtandao kama vile Facebook, Instagram, WhatsApp, YouTube, Barua Pepe, pamoja na huduma nyingine zinazopatikana kwenye KaiStore.”

Myonga pia ameongeza kusema kuwa uzinduzi wa simu hii mpya katika soko la simu za mkononi nchini Tanzania kutaongeza thamani na kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini na hivyo kuongeza ubora wa maisha kwa watanzania wote. “Pamoja na kuwapa huduma zenye ubora wa hali ya juu wateja wetu na kwa gharama nafuu, Simu hii ya TECNO Kitochi itasaidia kupunguza wimbi kubwa la watu wasioweza kupata huduma za kidigitali nchini kwani simu hii ni ya gharama nafuu ikiwa na vigezo na sifa zote za simu janja ya 4G. Ni matumaini yetu kuwa sasa watanzania wote wataweza kupata huduma zetu za mtandao wenye kasi ya 4G na kupata huduma zetu zote za kidigitali. Ni mpango mkakati wetu kuhakikisha hakuna mtanzania anayebaki nyuma linapokuja suala la kutumia huduma bora za kidigitali.”

Kwa mujibu wa Myonga, “Simu zetu hizi mpya sasa zinapatinaka katika maduka yetu yote nchini na kwa mawakala pamoja na wabia wetu nchi nzima, pia simu hizi zitapatikana zikiwa na ofa ya FACEBOOK BURE kwa miezi 12.

TECNO T-Smart 4G, ni simu yenye huduma zote kama za simu janja, na inaingia sokoni ikiwa tayari imesheheni apps zote maarufu za mitandao ya kijamii. Ni simu yenye uwezo wa 4G ambayo pia inaweza kufanya kazi kama WiFi kwa kuunganisha mpaka vifaa kumi kwa wakati mmoja. Hii ni simu inayotoa huduma zote muhimu na kwa viwango vya juu hususani kwa mteja ambaye hana uwezo wa kununua simu janja au kuhofia simu hiyo kuharibika ndani ya muda mfupi kutokana na aina ya kazi za mteja. Simu hii mpya itakuwa sokoni kwa bei ya hilingi 47,900/-, amesema” Myonga.

TAZAMA VIDEO HAPA TUKIO ZA UZINDUZI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad