Baraza la Uongozi kupitia kwa Rais wa Tanganyika Law Society, limewasiliana na Wakili Fatma Amani Karume ambaye amesema hakubaliani na uamuzi wa yeye kuondolewa kwenye Orodha ya Mawakili Tanzania Bara na yu tayari kukata rufaa
Baraza la Uongozi limeazimia kwa kauli moja kutoa msaada wake kwa mwanachama wake, Fatma kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo na litampa msaada wote wa kisheria litakaloweza katika rufaa yake na hii ni baada ya Baraza kuguswa na yafuatayo:
(1) Mwanasheria Mkuu aliwasilisha upya malalamiko yake kwa Kamati ya Mawakili kinyume na amri na maelekezo ya Jaji Kiongozi, Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi aliyoyatoa katika kesi ya Ado Shaibu Vs. Rais John Joseph Pombe Magufuli
(2) Muundo wa Kamati hiyo ya Mawakili kusikiliza lalamiko lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu dhidi ya Fatma Karume una uwezekano mkubwa wa kuwepo kwa upendeleo au muonekano wa upendeleo
(3) Kupokelewa kwa ushahidi wa kieletroniki wakati shauri linaendelea ambao haukuambatanishwa kwenye lalamiko au katika Orodha ya Nyaraka zitakazotumiwa (kama ilikuwepo)
(4) Ukubwa wa adhabu na ukali wa adhabu na (5) Taathira ya uamuzi huo kwa uwakili/utetezi na Uhuru wa Mawakili Tanzania Bara