Mamlaka ya hali ya hewa nchini,(TMA), imetoa muelekeo wa mvua za msimu za mwezi Novemba 2020 hadi April mwaka 2021 ambapo imeeleza uwepo wa mvua za wastani katika nyanda za magharibi Na mvua za wastani hadi wa chini kwa upande wa magharibi.
Akitoa maelezo katika mkutano na waandishi wa habari leo, kuhusiana na utabiri huo Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk.Agness Kijazi, amesema kuwa mvua hizo zinatarajiwa kuanza mwezi wa Novemba na kuisha katika mwezi wa nne huku muda wa kuanza mvua hizo unatofautiana kulingana na maeneo husika.
Akizungumzia juu ya athari zitakazo tokana mvua hizi za misimu kwa upande wa kilimo amesema unyevunyevu wa udongo na upatakinaji wa maji kwa ajili ya kilimo itakuwa yakuridhisha katika maeneo mengi hivyo amewataka wakulima kuzitumia mvua kwa ajili ya kufanya uzalishaji wenye tija.
Aidha Mamlaka hiyo imewatahadharisha wakazi waliopo maeneo hatarishi kuchukua tahadhari ilikuepukana na athari zinazoweza kujitokeza kufuatia mvua hizo za msimu.
"Vipindi vya mvua kubwa vinaweza kusababisha kutuama kwa maji na mafuriko na kupelekea uharibifu wa miundombinu na upotevu wa maisha na mali,mamlaka za miji na wadau wengine wanashauriwa kuboresha mifumo ya kupitisha maji taka na kuisimamia ili kupunguza athari zinazoweza sababisha mafuriko"
Aidha Mamlaka hiyo imetoa tahadhari kwa wavuvi na mamlaka za miji juu ya athari zinazoweza kujitokeza katika msimu wa mvua unaotarajiwa kuanza kuanzia mwezi Novemba 2020.