Trump akataa kushiriki mdahalo na Mpinzani wake Biden Oktoba 15



Rais anaye maliza muda wake nchini Marekani na mgombea urais wa cha Republican, Donald Trump amesema hataki kushiriki mdahalo na Joe Biden kama sehemu ya kampeni ya uchaguzi wa urais nchini Marekani, kama inavyopendekezwa na kamati ya mdahalo kwa wagombea urais.


Kulingana na muundo huu wa pande mbili, mdahalo wa pili miongoni mwa mitatu kati ya wawili hao, Oktoba 15, kwa ajili ya uchaguzi wa urais wa Novemba 3 nchini Marekani, ulitarajiwa kufanyika wakati wawili hao wakiwa wamekaa kila mmoja mbali na mwengine, kama tahadhari ya kiafya, wakati rais aliambukizwa virusi vya Corona.


Mdahalo huu ungefanyika mbele ya umati wa watu, ambao wangeliuliza maswali kwa wagombea wote, chini ya usimamizi wa Steve Scully katika eneo moja huko Florida, na Donald Trump pamoja na Joe Biden wangeliwajibu wakiwa mbali n wao, tume inayosimamia midahalo ya wagombea urais imebaini.


Uamuzi huo umechukuliwa ili "kulinda afya na usalama wa wote ambao wangelishiriki na kuhudhuria mdahalo," tume hiyo imeongeza katika taarifa.


Kwenye kituo cha Fox Business Network, Donald Trump amejibu: "Sitafanya mdahalo kama huo."


"Sitapoteza wakati wangu na mdahalo kama huo, hiyo sio kile ninachokiita mdahalo," amekiambia kituo hicho kwa njia ya simu. "Tunakakiwa kuketi nyuma ya kompyuta na kila moja kutoa sera zake na kujibu maswali: huo ni ujinga kabisa, kwa kutumia utaratibu huo wanakukata wakati wowote wanapotaka."


Timu yake ya kampeni imeongeza kuwa angefanya mkutano wa kampeni badala ya kushiriki kwenye televisheni ana kwa ana.


Kwa upande wake, Joe Biden amebaini kwamba atafuata sheria zilizowekwa na tume na hajasema juu ya kufanyika kwa mdahalo huu Oktoba 15.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad