Tuwalinde Watoto Dhidi Ya Ukatili – Msajili Mahakama Kuu



Hakimu Mwandamizi Rhoda Ngimilanga akichangia mada kwenye semina hiyo.

Jamii imeaswa kuonesha ushirikiano pindi mtoto anapofanyiwa ukatili ikiwemo kupigwa, kubakwa na kulawitiwa ili kuwalinda na kupata Taifa bora la badaye.

Hayo yamesemwa mapema leo na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Nyigulila Mwaseba kwenye  semina ya ngazi ya jamii (GDSS) inayoandaliwa na mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP).

Amesema kuwa, kuna baadhi ya wanafamilia huwa hawatoi ushirikiano pale mtoto anapofanyiwa ukatili na kusababisha kesi kuishia hewani.

“Utakuta mtoto amebakwa au kulawitiwa, familia inakwenda Polisi kutoa taarifa vizuri, lakini wakija mahakamani, ushahidi unaotolewa ni tofauti.

Mmoja wa wadau akichangia mada kwenye semina hiyo.

Hii inatokana na kwamba wanafamilia pamoja na yule aliyefanya kitendo huwa wanakubaliana makubaliano yao, matokeo yake wakati kesi inaendelea, baadhi ya mashahidi hawaji mahakamani hivyo kesi inaishia njiani kabla mshtakiwa hajahukumiwa,” amesema Nyigulila.

Naye Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama Kuu, Rhoda Ngimilanga ameiasa jamii kupata msaada wa kisheria wakati wa kufungua mirathi endapo mmoja wa wanafamilia amefariki dunia.


“Akina mama mara nyingi huwa wanapata madhara endapo mume akifariki dunia.



Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Nyigulila Mwaseba akitoa somo kwenye semina hiyo.


Utakuta mmepata taabu kutafuta mali, lakini baba akishafariki dunia, watoto wanapata shida, mama anabaki hana pesa ya kulipia ada na hii ni kutokana na ndugu wa mume kupora mali.


“Kwa hiyo kuna utaratibu wa mirathi ambao unatakiwa kutumika endapo mume atafariki dunia, ni lazima cheti cha kifo kiwepo, kiitishwe kikao cha familia na mke wa marahemu lazima awepo, kijadili anayefaa kuwa msimamizi wa mirathi, kuandaa muhtasari kisha kupeleka mahakamani kufungua mirathi.



Mdau akichangia mada.


“Endapo mama ataona aliyeteuliwa akawa na shaka naye, atakwenda kuweka pingamizi la mirathi maana kuna wengine wakishakuwa wasimamizi huwa wanafikiri mali ni zao kama marehemu alikuwa na nyumba, basi yeye huwa anauza.


Hii hairuhusiwi yeye ni msimamizi tu, lakini mali zinawahusu watoto.” Alimaliza kusema hakimu Rhoda.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad