Tuzo za Grammy Zaibua Vurugu Wasafi!



DAR: Kitendo cha mastaa watatu kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) wakiongozwa na bosi wao, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ na Zuhura Othman ‘Zuchu’, kutangazwa kuwania tuzo kubwa duniani za Grammy kwa mwaka 2020, kimeibua vurugu kama zote.


 


Diamond au Mondi, Rayvanny na Zuchu, ndiyo wasanii pekee kutoka Afrika Mashariki, waliotajwa kwenye tuzo hizo, ambazo hufanyika kwa mwaka mara moja nchini Marekani.


 


Baadhi ya mashabiki wa lebo hiyo, wamekuwa wakivimba na wakijimwambafai mitandaoni, huku wakitamba kwamba, kwa sasa wasanii hao ni wa kiwango cha dunia au sayari nyingine ya muziki na siyo Bongo Fleva.


 


Mashabiki hao wameendelea ‘kuvuruga’ mitandaoni kwa kuandika namna ambavyo ni hatua ya kipekee, huku wakihamasisha ‘jeshi’ lao kubwa kuingia mzigoni kuwapigia kura.


 


Mondi ametajwa kwenye Kipengele cha Video Bora ya Mwaka Duniani, ambapo video zake mbili za Jeje na Baba Lao, zimeingia kwenye kinyang’anyiro.


Rayvanny yeye yupo kwenye Kipengele cha Albam Bora ya Mwaka Duniani, kupitia albam yake ya Flower.




Zuchu ambaye ni zao jipya kwenye muziki na Lebo ya WCB, yeye ametajwa kwenye kipengele cha Mwanamuziki Bora Chipukizi kwa mwaka 2020.


 


Sasa kazi ni moja tu; kuhamasishana kupiga kura kwa wingi, ili kuwa-surprise (kuwashangaza) waandaaji kwa kunyakua tuzo zote, bila kujali wanashindanishwa na wasanii gani wakubwa duniani.


 


Ikumbukwe kuwa, Tuzo za Grammy ndizo tuzo kubwa zaidi duniani na ili msanii aingie kwenye tuzo hizo, kuna hatua mbalimbali ambazo lazima azipitie.


 


Hatua ya kwanza ni msanii kutuma kazi zake kwa Academy (taasisi) ya Tuzo za Grammy ili ziweze kujadiliwa na kamati maalum ya waandaaji, kabla ya majina yao kuingizwa rasmi kwenye vipengele vya kuwania (nominations).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad