Villa yaendelea kupendwa bila uwepo wa Samatta



Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta, aliwafanya Watanzania wengi kuipenda na kuishabikia Aston Villa ya England, mara baada ya kusajiliwa katika dirisha dogo la msimu 2019-2020.



Wachezaji wa Aston Villa wakishangilia goli pekee lililofungwa na Ross Barkley dakika za mwishoni kabisa mwa mchezo


Pamoja na kutofanikiwa sana katika timu hiyo ya Aston Villa kama mchezaji, lakini alifanikiwa katika maisha ya nje ya mchezo, aliwaongezea wafuasi wengi katika mitandao yao ya kijamii, kwa mujibu wa tafiti inaonesha  Watanzania ndio waliongoza  kwa kujiunga na mitandao yao ya kijamii.


Kuondoka kwa Mbwana Samatta na kwenda kujiunga na  Fenerbahce ya Uturuki, kuliwafanya baadhi ya  mashabiki kutoka Tanzania kujiondoa katika mitandao yao ya kijamii kwa madai klabu haijamtendea haki na walipaswa kuendelea kumvumilia.


Lakini katika hali ya kushangaza, bado Watanzania wengi  wanaishabikia Aston Villa ambayo msimu huu, imeanza vizuri kwa kushinda michezo yote 4 mfululizo, ikiwemo ushindi wa kushangaza wa 7-1 dhidi ya mabingwa watetezi Liverpoo wiki iliyopita.


 Katika hali inayodhihirisha wapo Watanzania wengi  wanaoendelea  kuishabikia  Aston Villa, licha ya Samatta kuondoka, ni pamoja na shangwe zilizolipuka katika kumbi mbalimbali za kuoneshea mpira mara baada ya Aston Villa kupata  goli pekee katika mchezo dhidi ya Leicester City, Jumapili iliyopita na mchezo kumalizika kwa Villa kupata ushindi wa bao 1-0. Goli lilifungwa dakika ya 90 na Ross Barkley.


Mbwana Samatta akiwa Aston Villa amecheza mechi 14 za ligi kuu, akianza  mechi 11  na akiingia mechi 3 na kufanikiwa kufunga goli 1 tu. Kwenye michuano mingine alifanikiwa kufunga goli 1, hivyo kumfanya takwimu zake kuwa magoli 2 kwenye michezo 16.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad