Msanii wa HipHop Webiro Wasira ‘Wakazi’ ameshindwa kuchukua nafasi ya Ubunge ambalo alikuwa anagombea Jimbo la Ukonga kupitia Chama Cha ACT-Wazalendo ambalo limeenda kwa mshindi Jerry William Slaa kutoka Chama Cha Mapinduzi.
Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Ukonga amemtangaza Jerry William Slaa wa CCM kukalia kiti cha Ubunge baada ya kupata kura 120936 sawa na asilimia 81.2 na msanii Wakazi Webiro Wasira kutoka ACT-Wazalendo amepata kura 2087 sawa na asilimia 1.4
Aidha Jimbo hilo la Ukonga kutoka Halmashauri ya Manisapaa ya Ilala lilikuwa na jumla ya wagombea Ubunge 18.
Msanii Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana Fa amefanikiwa kushinda nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Muheza,Tanga kupitia Chama Cha Mapinduzi ‘CCM’ akimshinda mpinzani wake Yosepher Komba wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’.
Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Muheza, amemtangaza Mwana Fa wa CCM kuwa ndiye mshindi wa nafasi ya ubunge wa Jimbo hilo baada ya kupata kura 47,578 na kumshinda Yosepher Komba wa CHADEMA aliyepata kura 12,034.
Mwana Fa anaungana na wasanii wengine ambao waliingia Bungeni kama Joseph Mbilinyi aliyeshindwa kutetea nafasi yake ya Ubunge Jimbo la Mbeya Mjini na Joseph Haule ‘Prof Jay’ aliyeshindwa nafasi ya Ubunge Jimbo la Mikumi.
Watu wengi wamempongeza Mwana Fa kwa matokeo hayo akiwemo mtu wake wa karibu na msanii AY ambaye kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kuwa “Ni Mheshimiwa Hamisi Mwinjuma ‘Mwana Fa’ kwenye moja na mbili hongera, hatimae ndoto yako ya muda mrefu ya kuwatumikia ndugu zako wa Muheza, kila la kheri mwanangu maana nakuaminia kwenye mipango ya kimaendeleo, Mungu ni mwema sana sasa kazi ianze”
Lakini pia Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Buchosa amemtangaza Mgombea Ubunge Jimbo hilo Kupitia CCM Erick Shigongo @ericshigongo kuwa mshindi kwa kupata kura 79,950 akifuatiwa na Abbas Mayala (CHADEMA) kura 11,285.
Watu wengine waliopo kwenye tasnia ya Muziki ni pamoja na Babu Tale aliyeshinda katika jimbo la Morogoro Kaskazini huku Profesor Jay jimbo la Mikumi, Joseph Mbilinyi Sugu jimbo la Mbeya mjini na wote Chadema wakishinda kwenye Ubunge.