Wagombea wa majimbo ya Tarime mjini na vijijini kufunga kampeni leo

 


Leo ni siku ya kufunga kampeni za uchaguzi kwa wagombea wa majimbo ya Tarime mjini na vijijini huku wanawake miamba (3) Chadema wakiwasha moto majimboni kwa kuwasihi wapiga kura kuwachagua ili kuwawakilisha Bungeni.


Esther Matiko Mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini jana alilaani kitendo cha baadhi ya vijana kuponda gari lake mawe kwa lengo la kudhoofisha nguvu za kampeni.


Matiko alisema kuwa kitendo hicho ni cha kinyama na cha kiuonevu na hakikubaliki kwa binadamu mwenye akili timamu kuponda gari mawe badala ya kueleza sera ya chama chake kuwa wakifanikiwa watawafanyia nini wananchi.


Matiko aliongeza kuwa kitendo cha gari kupondwa  mawe kipindi hiki cha kampeni jana ameripoti polisi ili kuchukua hatua na sasa anasuburi hatua kuchukuliwa ili waliofanya kitendo hicho kuchukuliwa hatua za kisheria.


Matiko alitumia nafasio hiyo wananchi kum,wamini na kumchagua tena ili kwewnda bungeni nan kuwatumikia ambapo alisema kuwa wapiga kura wapuuze ambao wanasema hajafanya kitu kwa mika mitano aliyokabidhiwa ubunge.


Kwa upande wa mgombea ubunge jimbo la Serengeti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Catherina Ruge hivi karibuni alikutwa na mkasa na vyombo vya habari vikaripoti,lakini sasa anasema serekali itaingilia kati vitendo hivyo ili kuhakikisha haki inatendeka na wale ambao wanania mbaya wanachukuliwa hatua.


Ruge anawaomba wapiga kura kumchagua na kiuwa mwakilishi wao Bungeni ili kuwasemea watu wa Serengeti na kero zao kutatuliwa siovinginevyo.


Mbali na Rugee wa Serengeti kuna mwamba mwanamke kutoka Jimbo la Bunda mjini Chadema,Esther Bulaya ameonyesha ujasiri na kuomba kura kwa wapiga kura kuwaamini wanawake kwasbabu hata ndani ya serikali wanawake wameonyesha mfano wa kuwa wanaweza tofauti na wanaume.


Ukija Tarime mgombea ubunge viti maalumu,Tekra Johanes aliwataka wapiga kura kujitokea kwa wingi kwenda kupiga kurua na kuwachagua viongozi wanaotokana na Chadema kwasbabu CCM imeongoza mwiaka mingi tangu uhuru kwa hali hiyo wananchi waende kukiamini chama chake na kukipa ridhaa ya kushikila nchi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad