1. Dwayne Johnson – Mapato yake ni dola Mil 87.5
Dwayne Johnson The Rock’, muigizaji wa filamu Mmarekani mwenye asili ya Canada ndio aliyevunja rekodi ya kuwa mwigizaji tajiri zaidi duniani mwaka huu ikiwa ni mwaka wa pili mfululizo, kulingana na orodha ya utajiri ya jarida la Forbes.
Pia inasemekana kwamba mapato yake ni dola milioni 87.5 kwa mwaka, makubaliano yake ya hivi karibuni yakiwa ni dola milioni 23 ya kufanya filamu na mtandao wa Netflix.
Dwayne Johnson alifuata nyayo za baba yake Rocky na kuwa bondia. Alikuwa na mafanikio makubwa kwenye ubondia kabla ya kugeukia uigizaji, na kuwa nyota kwenye filami ya Scorpion King, Fast & Furious 6 na kampuni ya Jumanji.
2. Ryan Reynolds – Mapato yake ni dola Mil 71.5
Muigizaji Reynolds, mtengenezaji filamu wa Marekani ambaye mapato yake ni dola milioni 71.5 kwa mwaka, kulingana na jarida la Forbes.
Alitengeneza zaidi ya dola milioni 20 kutoka kwa filamu moja tu.
Filamu zake za hivi karibuni ni pamoja na Free Guy, The Croods: A New Age na The Hitman’s Wife Guard.
3. Mark Wahlberg – Mapato yake ni dola Mil 58
Mark ni mwigizaji wa Marekani, mchekeshaji na mtayarishaji filamu wa Hollywood. Filamu moja aliyotengeneza imekuwa ya tatu kwa orodha ya zilizotazamwa sana katika mtandao wa Netflix.
Mark Wahlberg
Alitengeneza mamilioni ya madola kwenye filamu za vichekesho. Mapato yake kwa mwaka yanasemekana kuwa dola milioni 58.
4. Ben Affleck – Mapato yake ni dola Mil 55
Amefanikiwa kuingiza kipato kikubwa sana alipoachia filamu yake inayojulikana kwa jina la The Way Back na kufanya kuwa na mkwanja mrefu mno hali iliyopelekea kuingia katika orodha hii
5. Vin Diesel – Mapato yake ni dola za Kimarekani Mil 54
Angalau kwa kiasi fulani Vin Diesel mwaka huu ameweza kuingiza mapato ya dola milioni 54 mwaka huu na kumfanya kuwa nafasi ya tano kwenye orodha hiyo.
6. Akshay Kumar – Mapato yake ni dola Mil 48.5
Muigizaji wa India Akshay Kumar amekuwa miongoni mwa waigizaji 10 wanaolipwa vizuri zaidi duniani mwaka huu.
Akshay, mmoja wa waigizaji maarufu huko Bollywood, ameigiza zaidi ya filamu 100 katika kipindi cha miaka 30 iliyopita.
Mapato yake ni dola milioni 48.5 kwa mwaka. Amekuwa muigizaji pekee wa India kuingia miognoni mwa waigizaji 10 matajiri duniani.
Utajiri wake mkubwa unasemekana kwamba umetokana na matangazo ya biashara kwa makampuni makubwa makubwa kote duniani. Sasa hivi anafanyia kazi filamu inayofahamika kama Belbotom.
Pesa za Akshay zinatokana na mikataba yake kwenye uigizaji na biashara za kibinafsi kunakojumuisha tuovuti ya maonesho inayojulikana kama “The End”.
Muigizaji huyo kila wakati amekuwa mstari wa mbele akilinganishwa na waigizaji wengine, tajiri na mwenye ushawishi katka jamii.
Akshay pia ni wa 52 katika orodha ya watu mashuhuri ya Forbes. Watengenezaji filamu wa Hollywood inasemekana kwamba wako mbioni kumjumuisha Akshay kwenye filamu zao.
7. Lin-Manuel Miranda – Mapato yake ni dola Mil 45.5
8. Will Smith – Mapato yake ni dola Mil 44.5
9. Adam Sandler – Mapato yake ni dola Mil 41
10. Jackie Chan – Mapato yake ni dola Mil 40
Muigizaji anayetoka Hong Kong, China na anafahamika kwa filamu zake za maudhui ya vita na vichekesho.
Alitengeneza zaidi ya filamu 5 mwaka jana na kupata mapato ya zaidi ya dola milioni 40.
Licha ya mapato yake ya juu kutokana na matangazo ya biashara, ndio mwigizaji wa pekee kutoka China kuwa miongoni mwa waigizaji matajiri zaidi duniani.