Hayo aliyasema katika Ukumbi wa Bariadi Conference Center ulioko halimashauri ya mji wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu akizungumza na wadau kutoka asasi mbalimbali zinazosimamia uzalishaji na ununuzi wa zao la pamba ndani ya nchi.
Bashe aliwataka wadau kutoka benki zote Nchini kutumia mifumo ya kisasa wanapokua wakitoa mikopo kwa wakulima pamoja na kutenga fedha mahususi ili kuwawezesha vijana waliojiajiri katika kilimo wanatimiza ndoto zao kwa kuwapa mkopo wenye riba nafuu.
Aidha Bashe amezipongeza AMCOS kwa shughuri zote wanazozifanya ilikuhakikisha mkulima anapata elimu ya uzalishaji wa zao hilo, na kuwataka wadau wanunuzi wa pamba kutoka makampuni mbalimbali nchini kuweka mikataba na AMCOS ili kuwa na makubaliano sahihi ya being katika kuuza zao la pamba.
"Kwanza niwapongeze wakulima wa pamba mkoa wa simiyu, lakini pia niagize mamlaka wakulima walio ingia katika mfumo mashamba yao yapate hati za kimila kumiliki mashamba hayo," alisema na kuongeza kuwa:
"Niwaombe AMCOS kupitia Bodi ya pamba, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na vyama vya ushirika ikiwezekana viingie mkataba wa makubaliano na wadau Wanunuzi wa pamba na kila AMCOS iwe na kampuni lake
ili kuweza kuwakopesha wakulima kirahisi". Alisema Bashe.
Bashe aliongeza Kwa upande wa Benki niwaombe waanze kutumia mfumo wa kidigital na kuachana na mifumo iliyopitwa ilikuwakopesha wadau wa zao la pamba kwani inapunguza tozo katika riba na mikopo iwe katika AC model tofauti na Normal model.
"Aidha Tumajipanga kugawa mifuko ya kuvunia na kuhifadhia kwa wakulima wote, zawadi ya trekta kwa mkulima atakayefanya vizuri zaidi, na tunatarajia kupima afya ya udongo nchini kote na bila kusahau GASPI nimewaomba watengeneze vitambulisho vyenye jina la mkulima, picha, jina la Kijiji na halimashauri husika ili kumtambua mkulima kirahisi zaidi".
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka amewataka maafisa wote wa kilimo na wakuu wa wilaya katika halmashauri zote kuhakikisha wanalipa madeni ya wakulima wote kufikia ijumaa, kwani fedha za madeni yote zimeshaweka katika akaunti ya kila halmashauri.
Kupitia Viongozi wa AMCOS vyama hivyo vimeweza kutoa mapendekezo pamoja na maoni ya jinsi ya kumsaidia mkulima kupitia utafiti pamoja na kutoa elimu juu ya uzalishaji wa zao la pamba ilikumwezeshakuzalisha kwa ubora zaidi.
"Ili kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa zao hili ninashauri viongozi wa AMCOS wapewe nafasi kwani ndiyo wanaojua changamoto zinazomkabili mkulima, pili tafiti zifanyike kwa wakulima moja kwa moja na mwisho serikari naiomba wamtambue mkulima anayefanya vizuri hata kwa kumpa zawadi hii itaongeza ushindani zaidi". Alisema Emmanuel William (katibu AMCOS Bima la maji).