Wanamgambo wa Al-Shabaab washambulia msafara wa kijeshi Somalia, wanajeshi 13 wauawa



Wanajeshi 13 wameripotiwa kupoteza maisha baada ya msafara wao wa kijeshi kushambuliwa na wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab nchini Somalia.

Kulingana na taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari vya ndani, Meja Mohammed Ali aliarifu kuwa msafara wa kijeshi ulishambuliwa na Al-Shabaab kwenye maeneo ya Afgoye yalioko umbali wa kilomita 30 kutoka kusini magharibi mwa mji mkuu wa Mogadishu.


Wakati wa mashambulizi hayo, ufyatulianaji risasi ulitokea kati ya wanajeshi wa Somalia na wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab ambao walikuwa wengi kwa idadi.


Ali alisema, ‘‘Wanajeshi 13 wamepoteza maisha kwenye mashambulizi hayo yalitotekelezwa na wanamgambo wa Al-Shabaab.’’


Jeshi la Somalia limetangaza kushika doria na kudhibiti usalama katika eneo hilo lililokumbwa na mashambulizi.


Msemaji wa kundi la Al-Shabaab Abu Musab ametoa madai ya kuuawa kwa wanajeshi 24 kwenye mashambulizi.


Kundi la Al-Shabaab lilioundwa mwaka 2004, limekuwa likidhibiti maeneo ya kusini mwa nchi ya Somalia.


Wanamgambo wa kundi hilo wamekuwa wakishambulia taasisi za serikali, hoteli na vikosi vya usalama katika miji mbalimbali.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad