Sophie Pétronin, 75, alitekwa nyara nchini Mali Desemba 2016Image caption: Sophie Pétronin, 75, alitekwa nyara nchini Mali Desemba 2016
Familia ya raia wa mwisho wa Ufaransa aliyetekwa nyara na wanamgambo wa Kiislamu nchini Mali imesema ameachiliwa huru.
Familia hiyo imethibitisha Sophie Pétronin – mwenye umri wa miaka 75, mfanyakazi katika shirika la kutoa msaaada – yuko njiani anaelekea mji mkuu wa Bamako – Ingawa serikali ya Ufaransa bado haijathibitisha hilo.
Bi. Pétronin alitekwa nyara na kundi la kigaidi la al-Qaeda- lenye kuhusishwa na wanaume wenye silaha kaskazini mwa mji wa Gao ambako amekuwa akiendesha shirika la kutoa msaada.
Soumaïla Cissé alitekwa nyara akiwa kwenye msafara wa kampeniImage caption: Soumaïla Cissé alitekwa nyara akiwa kwenye msafara wa kampeni
Taarifa huko Mali zinasema kwamba raia mwingine aliyeshikwa mateka mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa mgombea urais Soumaïla Cissé, 70, pia nae ameachiliwa huru na wanamgambo hao.
Mwanasiasa huyo amekuwa akizuiliwa tangu mwezi Machi.
Inasemekana kwamba kuachiliwa kwao huru ni sehemu ya makubaliano yanayojumuisha kuachiliwa huru kwa wapiganaji wa jihadi zaidi ya 100 na mamlaka.