Baada ya matokeo kutangazwa ya kuwa kwa awamu ya pili Dkt. John Pombe Magufuli anaenda kuliongoza taifa la Tanzania tena na watu wengi kumpongeza kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii
Wasanii Alikiba na Harmonize hawakuwa nyuma na wao wamempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa na wananchi kulingooza taifa la Tanzania kwa mara nyingine tena.
Kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii wameandika haya.
ALIKIBA.
Hongera kwa ushindi wa kishindo Mheshimiwa Rais Mteule, Dr John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mteule @samia_suluhu_hassan. Watanzania tumeonyesha imani kubwa nanyi kwa kuwaongezea miaka mengine 5 ya kuliongoza taifa letu, nawaombea kwa Allah awaongoze katika kila hatua ya uongozi wenu kwenye taifa hili, muongoze kwa amani, upendo na busara zaidi katika kuisogeza Tanzania katika maendeleo makubwa zaidi. Mwenyezi Aibariki Tanzania 🇹🇿, Dr John Pombe Magufuli na viongozi wote waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu. Tudumishe Amani na Upendo. @asas_dairies @ccmtanzania. @hpolepole @gersonmsigwa
#MagufuliTanoTena
#KingKiba
HARMONIZE.
Happy birthday Mr president 🎉🎈🎆🧨 Pole Kwa Uchovu wa Kuzunguka Kila Chochoro Kuzinadi Sera Tukufu na Hatimae Tumeshinda Kwa Kishindo Hongera Sana ….!!!! DR JOHN POMBE MAGUFULI rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania 🇹🇿 Kazi Ziendele…!!!!! 🏁 We made History Together 🛀🛀 Na Kesho Tutasherehekea Hapa KONDEGANG H.Q #USHAMBANIGHTPARTY 🏁🏁🏁🏁