Wasanii kushiriki kampeni, tusitegemee Muziki wetu kwenda Kimataifa

 


Wasalamu Wakuu.

Naomba Ieleweke kuwa Sisi Kama Tanzania mziki wetu kutoboa Kimataifa Bado Sana Na Tuna Safari Ndefu Mnooo. Hatuwezi Kukaa Kuwa Sawa kama Nigeria, SA na Nchi zingine Zilizotoboa Kimataifa. Hivyo Wasanii Watanzania Nina amini Wanakazi Kubwa Sana Kuhakikisha Mziki Wetu unakuwa Mziki Pendwa Nje ya Tanzania Na Nje Ya Afrika.


Lakini Nachelea Kuamini kama wasanii Wetu Wanaelewa Wanachokifanya Na Kama Sisi Watanzania Tunahitaji Sana Kwenda Kimataifa Kuliko Hii Local.


Kule Ambako tunataka mziki Wetu Uende Kimataifa Tunatambua Ni Watu Wa Aina Gani Wale? Oky Ieleweke kuwa Wale Watu Wametuzidi Kila Kitu kuanzia Mitazamo, Fikra, Utendaji kazi Na Vitu Vingine Vingi. Huwa Ni Watu wakupambanua mambo kuchambua na Kufanya Maamuzi.


Kitendo Cha Asilimia 90% ya Wasanii Wetu Kushiriki Kampeni za Kisiasa Zinaondelea Tanzia Na Ushiriki wao ni Zaidi ya 89%, Hii inadhihirisha kwamba wasanii Wetu hata wale Tunao Wategemea Kutusua Zaidi Kimataifa Hawajui Walifanyalo Na Hawajuii Thamani Yao. Tusitegemee Tuzo Za Kimataifa Zitaona Wasanii Wetu Kama Ni Best Performers Kupitia Hizi Perfomance za Kwenye Kampeni Ambako Kiingilio ni Miguu Yako, Tusitegemee Mziki Wetu Utaenda Kimataifa Kwa Vyombo Vya Mziki Vilivyopo Kwenye Majukwaa haya Ya Kampeni ambavyo Vitanatoa Sauti Mbovuu Kupitiliza Zaidi Zaidi Ni Kujishusha, Hata Kama Mgombea Anapendwa Kimataifa Au Hapendwi.


Lakini Hizi Show za Kwenye Kampeni Inashirisha Ukweli Kwamba Wasanii wa Bongo Maisha Yao ni Magumu sana Bila Show, Mtu Atajituma Kuwa Na Wimbo Mzuri Tanzania Ili Apate Show Za Kwenye Kampeni Lakini isiwe Kwenda Kimataifa, Inasikitisha Sana.


Kule ambako Mziki Wetu Tunataka Ufike Sio Waumini Sana Wa Siasa Au Serikali Iyopo Madarakani Ni Watu wa Kusimamia Haki Na Ukweli. Mfano Mzuri Ni DAVIDO na WIZKID kwenye Issue Ya SARS, Kitu Ambacho Wasanii Watanzania Hawataweza Kuja Kufanya Kwasababu Watu ni sehemu Ya Watu Walioshiriki kufanya Kampeni hivyo sisi Kama Watanzania Tusitegemee kama Wasanii au Mziki Wao Utakuja Kutusaidia Katika Kutetea Haki Zetu pale Itakapotokea Issue kama SARS kule Nigeria.


Lakini Mwanasiasa Ni Nani? Mwanasiasa ni mtu anaehitaji kutimiza Mambo Yake ndani Ya Miaka 5 tuu baada ya Hapoo Hakutambui Tena. Msaada Wanao utoa Wanasiasa Kwa Sasa Kwa Wasanii hawatautoa Wasipokuwa Madarakani. Wasanii Wetu Management zao Zinakosa Uelewa Na Zinakosa Umakini Katika Kusimamia Wasanii Wao. kitendo Cha Wasanii kushiriki kampeni ni Ishara pia Wasanii wetu wana Management Mbovu sanaa...


Hivi Kuna Nchi ambayo Wasanii wanashiriki kampeni Kama TanzaniA? Ni wapi Mziki Wa Tanzania Unaelekea? Tunapiga Hatua Moja Mbele na Kurudi Hatua Kumi Nyuma.


Tuwakumbe wasanii Wetu Wajibu wao

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad