Watu 42 wanusurika kifo baada ya basi la Mbeya City kupinduka eneo la Msoga Chalinze



ABIRIA wapatao 42 wamenususika kifo baada ya basi walilokuwa wakisafiria la kampuni ya Mbeya City lililokuwa likitokea mkoani Tanga kuelekea Mkoa wa Mbeya kuacha njia na kupinduka wakati dereva akijaribu kukwepa kundi  kubwa la ng’ombe ambao walikuwa wanavuka katika eneo la msoga halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa imeeleza kuwa tukio la ajali hiyo limetokea leo asubuhi majira ya saa 4;20 asubuhi na kwamba  wakati derava wa basi akijaribu kukwepa ndio alipopinduka na kusababisha mejuruhi  wajeruhi wapatao 11 ambapo kati yao wanaume ni watatu na wanawake nane.


Pia Kamanda huyo ameeleza kuwa  majeruhi hao afya zao sio nzuri sana na wamekimbizwa katika kituo cha afya msoga kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi na hakuna abiria yoyote ambaye amepoteza maisha katika ajali hiyo n kuongeza kwamba dereva wa basi hilo pamoja na mmiliki wa ng’ombe hao wametoroka kusikojulikana  na kwamba  jeshi la polisi linaendelea  na msako mkali kwa aajili ya kuwatafuta .


“Kwa sasa mareruhi wote 11  ambao wamepata ajali katika eneo la  wanaendelea kupatiwa matibabu zaidi katika kituo cha afya Msoga na kwamba chanzo cha ajali hii ni kundi kubwa la mifugo aina ya ng’ombe  ambao walikuwa wakivushwa katika barabara hiyo na katika harakati za dereva wa basi kutaka kuwakwepo ndipo basi hilo lilipopinduka,”alisema Nyigesa.


Kadhalika Kamanda huyo alitoa wito kwa madereva wote na watumiaji wengine wa barabarani kuhakikisha kwamba wanachukua tahadhari pindi wanapokuwa wanataka kuvuka katika barabara za umma na kuzingatia sheria taratibu na alama zote ambazo zimewekwa barabarani.


Pia Kamanda huyo alisema kuwa kufiatia kutokea kwa ajali hiyo wanaendelea na msako mkali wa kuwatafuta watu wawili ambao ni dereva wa basi hilo ambaye alikuwa amepakia abiria huku akiwa katika mwendo wa kasi pamoja na mmiliki wa mifugo hiyo ambao wamekimbia pasipojulikana,

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad