Yanga Kigelegele: Mashabiki Punguzeni Mihemko Viwanjani



Mhariri wa Championi Ijumaa, John Joseph (kulia) akimsikiliza Yanga Kigelegele baada ya kumpachika swali. Shabiki huyo maarufu wa Yanga alitembelea ofisi za gazeti hilo zilizopo Sinza Mori jijini Dar, juzi.


SHABIKI maarufu wa Yanga, Anuary Wambura ‘Yanga Kigelegele’, amewataka mashabiki wa Simba na Yanga kupunguza mihemko wanapokuwa viwanjani ili kuepuka vurugu zisizo za lazima.


 


Katika siku za hivi karibuni, kumetokea vurugu viwanjani zilizohusisha mashabiki wanaotajwa kuwa ni wa Simba na Yanga hali ambayo kila mmoja amekuwa akikemea ikiwemo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).


 


Shabiki huyo ambaye mapema wiki hii alitembelea Ofi si za Gazeti la Spoti Xtra zilizopo katika Jengo la Global Group, Sinza Mori jijini Dar, alisema: “Mashabiki wakae wakifahamu kuwa, soka ni burudani na si uadui, wanatakiwa kuwa kitu kimoja.



Yanga Kigelegele akiwa katika pozi ndani ya studio za Global TV Online.


“Mfano katika tukio lililotokea kwenye mechi yetu dhidi ya Mtibwa Sugar kule Morogoro, nilikuwepo uwanjani na nilishuhudia kila kitu, masabiki wa Simba walikuwa wametoa lugha ambazo si za kiuanamichezo kwa mashabiki wa Yanga ndio maana walichukua maamuzi yale japo mimi mwenyewe nalaani matukio twendeni uwanjani kwa utulivu hata kama utani utakuwepo uwe wa kawaida na kuleta furaha na si kama yale, sipendi kuona mashabiki wanakuwa maadui.


 


“Watu wanatoa lugha za kejeli wanapokuwa uwanjani ambazo zinawaumiza mashabiki wengine jambo ambalo si sahihi kwani inapelekea kuchochea hasira, hivyo tujaribu kuangalia lugha tunazotoa.“Mashabiki wanatakiwa kupunguza mihemko na kutoa lugha ambazo zitawakera wengine, kuzua chuki.



Mtangazaji wa +255 Global Radio, Kisa Daniel, akiwa katika pozi na Yanga Kigelegele.


”Yanga Kigelele ambaye ni maarufu kwa staili yake ya kushangilia kwa kupiga vigelegele, alipokuwa Global Group, alipata muda wa kutembelea idara zote ikiwemo kitengo cha magazeti ya michezo, Spoti Xtra na Championi, Global TV Online na +255 Global Radio, kisha kufanya mahojiano maalum.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad