Yanga SC Yamtema Mzungu Wake



BAADA ya kimya kutanda kwa muda mrefu, hatimaye Klabu ya Yanga imefi kia makubaliano ya kuachana na aliyekuwa kocha wa viungo wa timu hiyo, Msauz, Riedoh Berdien.

Ikumbukwe Riedoh aliondoka nchini kabla ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar na Coastal Union na kurejea Afrika Kusini kwa ajili ya mapumziko ya wiki moja, lakini tangu alipomaliza muda wake wa mapumziko mafupi, alishindwa kurudi Tanzania kuungana na kikosi cha Yanga baada ya kukosa ushirikiano kutoka kwa viongozi wa timu hiyo

Akizungumza na Championi Jumatano, Riedoh alisema kuwa, amekubaliana na uongozi wa Yanga kuachana na majukumu ya kuendelea kuwa kocha wa viungo wa timu hiyo baada ya baadhi ya viongozi wa Yanga kusema kuwa hawakumpa ruhusa ya kurejea Afrika Kusini kwa ajili ya mapumziko.

Riedoh aliongeza kuwa, wakati anaondoka kwa ajili ya mapumziko, alikubaliana na Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla, Hersi Said na kaimu katibu mkuu, Simon Patrick, lakini mshauri wa Yanga, Senzo Mazingisa, alikuwa hataki mtaalam huyo wa viungo arejee Afrika Kusini kwa ajili ya mapumziko.

“Wachezaji wengi na mashabiki walikuwa wananiambia hawataki niondoke, lakini nimefi kia makubaliano na viongozi wa Yanga niondoke kwa sababu walikuwa hawataki nirudi Tanzania, kilichonishangaza ni baadhi ya viongozi kusema sikuwa nimetoa taarifa kama nitaondoka kwa ajili ya mapumziko.

“Wakati naondoka nilikubaliana na Mwenyekiti, Mshindo Msolla, Hersi Said na Kaimu Katibu Mkuu, Simon Patrick, lakini kumbe Senzo alikuwa hataki mimi niende Afrika Kusini kwa ajili ya mapumziko na kuiona familia yangu, lakini wakati naondoka yeye hakuwepo Tanzania,” alisema Riedoh Berdien.

Riedoh alijiunga na Yanga msimu uliomalizika, mwezi Januari, mwaka huu baada ya jina lake kupendekezwa na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji Luc Eymael, lakini mkataba wa Riedoh na Yanga ulikuwa unatarajia kumalizika Januari, 2021.


Stori: Abdulghafal Ally, Dar es Salaam

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad