ALIYEKUWA Kocha wa Yanga, Mserbia, Zlatko Krmpotic ameibuka kuwa ameamua kwenda mwenyewe kwa miguu yake katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kuishitaki Yanga kutokana na kitendo cha uongozi wa klabu hiyo kuvunja mkataba wake bila kuwepo makubaliano yoyote.
Hivi karibuni, Yanga ilitangaza kumfuta kazi kocha huyo kutokana na kile kilichoelezwa timu kucheza kwa kiwango cha chini licha ya kushinda mechi zake, ambapo kwa sasa wanatarajia kumpa kazi Mrundi, Cedric Kaze aliyetarajiwa kutua nchini jana usiku.
Akizungumza na Championi IJumaa, Krmpotic alisema kuwa uongozi wa timu hiyo umevunja mkataba wake lakini hakuna makubaliano yoyote ambayo walisani, jambo ambalo halipo kitaaluma, hivyo ameamua kwenda FIFA mwenyewe baada ya kuwafungulia kesi ya madai ya fedha zake.
“Hadi leo (juzi) hawajasaini makubaliano yoyote ya kuvunja mkataba, hawajali kwa sababu wanajua fedha ninayowadai haitalipa klabu.
“Lakini atalipa bosi wao ambaye anafadhili kila kitu. Niliwashtaki FIFA na katika siku chache zijazo nitaenda mwenye makao makuu ya FIFA huko Zurich kwa ajili ya hili jambo hawajanitendea haki,” alisema Krmpotic.