Zuchu Aingizwa ‘Freemason’




DAR: Ohooo! Baada ya bosi wake kuandamwa mno na skendo nzito ya kuwa kwenye mwavuli wa jamii ya siri ya Freemason, mtoto mwenye sauti yake tamu kutoka pale Wasafi Classic Baby (WCB), Zuhura Othman ‘Zuchu’ naye ameingizwa kwenye mkumbo huo, IJUMAA limeinyaka!


 


Kupitia vyanzo mbalimbali, Gazeti la IJUMAA limefanikiwa kunasa madai mazito yanayomhusisha binti huyo anayesumbua na Wimbo wa Litawachoma na jamii hiyo ya siri, kwa kile kinachoelezwa kuwa, ameingizwa na bosi wake huyo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au ‘Mondi’.


 


“Mtoto wa nyoka ni nyoka. Wewe unategemea nini? Kama Mondi ni nyoka, Zuchu hawezi kuwa nyoka? Ni rahisi sana Mondi kuwa amemshawishi huyu mtoto ajiunge naye ili aweze kung’ara duniani,” chanzo kimoja makini kilinyetisha.




CHNZO CHAZIDI KUTIRIRIKA


Chanzo hicho kilikwenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa, mafanikio ya muda mfupi anayoyapata Zuchu kwa sasa, sambamba na suala zima la jinsi anavyokubalika kwenye jamii ndani na nje ya Bongo, inadhihirisha kwamba binti huyo tayari yupo kwenye jamii hiyo.


 


“Wewe angalia ndani ya miezi sita na ushee, kila mtu anazungumza Zuchu utadhani pale Wasafi hakuna wasanii wengine aliowakuta.


 


“Ndani ya muda mfupi, ameingia kwenye Top 100 za Billboard duniani, wakati hata bosi wake mwenyewe hajawahi kufikia hatua hiyo. Nyimbo zake zinatazamwa na kuwa trending nchini mpaka kero,” kiliongezea chanzo hicho.


 


VINYANG’ANYIRO VYA TUZO


Mbali na hayo, mafanikio mengine aliyoyafikia Zuchu ndani ya muda mfupi, ni pamoja na kuingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo zenye heshima kubwa duniani za Grammy za Marekani kupitia Kipengele cha Msanii Bora Chipukizi (The Best New Artist 2020).


 


Lakini kama hiyo haitoshi, Zuchu ametajwa pia kuwania Tuzo za African Entertaiment Awards USA (AEAUSA) katika kipengele cha Msanii Bora Chipukizi na pia kwenye Tuzo za Afrimma, ametajwa pia kuwania katika vipengele viwili; Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki na Msanii Bora Chipukizi 2020.




IJUMAA LACHIMBA ZAIDI


Gazeti la IJUMAA halikuishia hapo, liliingia kwenye vyanzo vingine, ambapo liliweza kunasa kurasa inayotajwa kuhusika na imani hiyo kwenye Mtandao wa Instagram ambayo ilionesha kuwa wanampongeza na kumkaribisha Zuchu ndani ya jamii hiyo.


 


UNAITWA FREEMASON WORLD


Kwenye ukurasa huo, wenye jina la freemason_world, waliweka picha ya Zuchu akiwa anaonekana na pete nne kwenye vidole vyake vinne na kusindikiza na ujumbe uliosomeka;


 


“Congratulations to @ officialzuchu on getting your benefits as a member of the Illuminati.”


Kwa tafsiri isiyo rasmi; “Hongera Zuchu kwa kupata faida kama memba wa Iluminati.” Illuminati inatajwa kushabihiana kwa karibu na jamii ya Freemason na zote ni jamii za siri zinazodaiwa kuhusisha makafara ya damu na kuwapa watu utajiri wa ghafla.


 


MAONI KAMA YOTE


Maoni mbalimbali kwenye ukurasa huo yameonesha kumpongeza Zuchu, huku wengi wakisema ni jamii nzuri ambayo haina shida na mtu tofauti na watu wanavyoifikiria.


 


Lakini hata hivyo, wapo wengine waliomuonya asiingie kwenye jamii hiyo, kwani haina mwisho mzuri zaidi wakamsihi amuamini Mungu.


Hata hivyo, taarifa nyingine zinadai kuwa, jamii hiyo ya Freemason kwa upande wa wanawake inazidi kushamiri kila kukicha, tofauti na ilivyokuwa zamani.


 


MONDI ANASEMAJE?


Mara kadhaa Mondi kupitia mameneja wake, Said Fella ‘Mkubwa na Wanawe’ na Hamisi Taletale ‘Babu Tale’, wamekuwa wakikanusha kuhusu mafanikio ya Mondi kuhusishwa na imani zozote za siri.


Wanasema kinachomfanya msanii wao huyo awe mkubwa na kazi zake zikubalike, ni juhudi zake binafsi, lakini pia, uongozi mzima wa WCB ambao ndiyo unaomsimamia yeye pamoja na wasanii wengine.




MONDI ANAMUINGIZA ZUCHU?


Gazeti la IJUMAA lilizungumza na Zuchu hivi karibuni ambapo hakutaka kuzungumzia madai ya kuingizwa Freemason, lakini aliongelea zaidi suala zima la yeye kudaiwa kubebwa na Mondi.


“Ndiyo nabebwa, lazima anibebe ndiyo. Kazi yake kama bosi, kumbeba msanii wake. WCB ni lebo ambayo inalea wasanii, hivyo ni lazima wafanye hivyo ili kutimiza majukumu yao,” alisema Zuchu.


 


REKODI ZA ZUCHU


Zuchu ana miezi sita na ushee tangu ajiunge na WCB, lakini nyimbo zake zimekuwa na mapokeo makubwa huko mjini YouTube, ambapo takwimu za juzi jioni, kwa baadhi ya nyimbo zake zilikuwa zinaonesha hivi;


Hakuna Kulala ilikuwa imetazamwa zaidi ya mara milioni 2.1, Kwaru (Mil. 4. 2), Wana (Mil. 8), Nisamehe (Mil. 6.4) na Mauzauza (Mil. 3.9).


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad