Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe amesema, wananchi wasitegemee kuwaona wabunge wa chama hicho bungeni na chama hicho kwa sasa hakiwazi suala la ruzuku au wabunge wa viti maalum.
Zitto amesema hayo leo Novemba 8, 2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho, Magomeni jijini Dar es Salaam, ambapo amesema zaidi ya wanachama 169 nchi nzima wamekamatwa katika siku ambazo zimepita na bado wanaendelea kukamatwa.
“Kwetu sisi hapakuwa na uchaguzi na kuna taratibu zinaendelea kufanywa ndani ya chama kwa wale waliotangazwa kushinda, lakini msitegemee kuona wabunge waliotokana na ACT-Wazalendo bungeni”, amesema Zitto.
“Hakuna jambo ambalo ni muhimu zaidi ya uhai wa watu, kiongozi mwenzangu (Mazrui) sijui anaendeleaje, sasa hivi siwazi ruzuku, viti maalum wala chochote, nachowaza ni damu ya wanachama wangu na uhai wa viongozi wangu”, ameongeza Zitto.
Katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, kati ya majimbo 264, ACT-Wazalendo ilijipatia majimbo manne ya Pemba-Zanzibar
Wewe dogo..!! Mbabaishaji.
ReplyDeleteKwa vipi.? Cha hiki cha Mbunge Mmoja
na Ofisi mfukoni kwenye Flashi.
Usijibabaishe na kubabaisha Watanzania
hivyo wewe wa wapi..???
Luzuku..Luzuku..!! Mwenyewe Falu Joni ukitaka mchongo kaa nae kitako.
Na ukitaka kuludi nyumbani M.V Amani ipo kazini.
Kumbuka Safari yako na Mzului haikuwa na Tija ila imewaumbua..Mkopo Tanzania iliupata.Roho yenu ya korosho imewauma
Tanzania ni ya Watanzania.
Mwenye kwa anaruka karibuni.na ww M.V Amani Umesha weka booking? Ushindwe.
TAMAA YA RUZUKU ITAKUPELEKA KULEEEE.!!
ReplyDeleteWewe Dogo..!! Mbabaishaji.
Kwani vipi.? Chama hiki cha Mbunge Mmoja na Ofisi mfukoni kwenye Flashi.
Usijibabaishe na kubabaisha Watanzania
hivyo wewe wa wapi..???
Ruzuku..Ruzuku..!! Mwenyewe Falu Joni ukitaka mchongo kaa nae kitako. au tumia bando na uongeze GB.
Na ukitaka kuludi nyumbani M.V Amani ipo kazini.
Kumbuka Safari yako na Mzului haikuwa na Tija ila imewaumbua..Mkopo Tanzania iliupata.Roho yenu ya korosho imewauma
Tanzania ni ya Watanzania.
Mwenye kwa anaruka karibuni.na ww M.V Amani Umesha weka booking? Ushindwe.