ACT-Wazalendo yatoa msimamo kwa wabunge wao



Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe amesema, wananchi wasitegemee kuwaona wabunge wa chama hicho bungeni na chama hicho kwa sasa hakiwazi suala la ruzuku au wabunge wa viti maalum.


Zitto amesema hayo leo Novemba 8, 2020  wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho, Magomeni jijini Dar es Salaam, ambapo amesema zaidi ya wanachama 169 nchi nzima wamekamatwa katika siku ambazo zimepita na bado wanaendelea kukamatwa.


“Kwetu sisi hapakuwa na uchaguzi na kuna taratibu zinaendelea kufanywa ndani ya chama kwa wale waliotangazwa kushinda, lakini msitegemee kuona wabunge  waliotokana na ACT-Wazalendo bungeni”, amesema Zitto.


“Hakuna jambo ambalo ni muhimu zaidi ya uhai wa watu, kiongozi mwenzangu (Mazrui) sijui anaendeleaje, sasa hivi siwazi ruzuku, viti maalum wala chochote, nachowaza ni damu ya wanachama wangu na uhai wa viongozi wangu”, ameongeza Zitto.


Katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, kati ya majimbo 264, ACT-Wazalendo ilijipatia majimbo manne ya Pemba-Zanzibar.

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Dogo..!!! Ulikuwa mbunge wa taasisi hii
    peke yako, Au kumbukumbu inakupotea?

    Huu utumbo unaozungumza mbona hauelewe

    Je unatambua kama Vilipukizi vimekamatwa visiwani..? Je unahusika.?

    Tunaendelea kuliangalia hili kwa kina
    huku tukilifanyia kazi mwengine atoroka na mwengine anatafuta hifadhi
    na wewe nae hatua inayofata ni new flashi ya GB64 , Amasivyo..??

    Dogo.!! mkopo Tanzania uliupata.

    Hivyo ulisafiri mkiambatana na Nani.?
    mpaka kwa mbutaNanga?

    Ughaibuni kuzuli , umesha tengeneza mazingira.?



    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau, Hii yote tamaa ya RUZUKU.
      Ruzuku mchezo? mtu yuko Radhi alale mlangoni usiku kucha kuingojea ruzuku. muulize mwenzako.!! kumchuzi na ugali.

      Delete
  2. Uta mtapelije Membe, tena bila haya.!!


    Dogo..!!! Ulikuwa mbunge wa taasisi hii
    peke yako, Au kumbukumbu inakupotea?

    Huu utumbo unaozungumza mbona hauelewe

    Je unatambua kama Vilipukizi vimekamatwa visiwani..? Je unahusika.?

    Tunaendelea kuliangalia hili kwa kina
    huku tukilifanyia kazi mwengine atoroka na mwengine anatafuta hifadhi
    na wewe nae hatua inayofata ni new flashi ya GB64 , Amasivyo..??

    Dogo.!! mkopo Tanzania uliupata.

    Hivyo ulisafiri mkiambatana na Nani.?
    mpaka kwa mbutaNanga?

    Ughaibuni kuzuli , umesha tengeneza mazingira.?



    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad