Afande Sele Awaambia Wasanii Waliokurupukia Siasa KISA Umaarufu na Kujikuta Wakiaibika Mbele ya Wajumbe

 


Msanii wa muda mrefu kwenye kiwanda cha muziki Bongo Selemani Msindi maarufu kama Afande Sele amesema kwenye mchakato wa uchaguzi mwaka huu amejifunza kuwa wajumbe hawaangalii sura,pesa au umaarufu wa ili kumpitisha kwenye uongozi.


Afande Sele ametoa mtazamo huo baada ya wasanii wengi kutia nia za kugombea Ubunge ila wameishia kukatwa na wajumbe huku wengine wakishindwa kwenye uchaguzi mkuu.

"Kuhusu wajumbe nilijifunza kwamba jamii ya watanzania hawamchagui mtu kwa sababu ya sura yake, umaarufu wake au pesa zake, huwa wanatazama mtu ambaye kimisingi atakuwa mwenzao kuanzia kushughulika naye na kuzunguka naye kwenye maeneo yote" amesema Afande Sele

"Kwa bahati mbaya wasanii waliingia kwenye mchakato huu hasa kwenye chama tawala wakitegemea sana umaarufu wa majina yao na sponsa waliokuwa nao kwamba watapata back up za pesa ya kampeni na wajumbe, lakini wananchi hilo ni jambo la mwisho kwao" ameongeza 


Wasanii ambao waliishia kukatwa na wajumbe ni Steve Nyerere, Mc Pilipili, Dkt Cheni, Master J, Mwijaku na Kingwendu na walioshindwa kwenye uchaguzi mkuu ni Prof Jay, Mr II Sugu na Wakazi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad