Ajichoma Moto Akipinga Rushwa



Mwanaume mmoja raia wa Misri amejichoma moto, kisha kuokolewa na polisi na wapita njia katika uwanja wa Tahrir, jijini Cairo, mtu huyo alifanya hivyo kupinga “rushwa na hali mbaya ya maisha”.


Mtu huyo alifukuzwa kazi katika benki kwa kuanika vitendo vya rushwa vilivyowahusisha maafisa wa serikali, kwa mujibu wa makala ya Middle East Eye.


Katika matangazo ya moja kwa moja ya Facebook, mwanaume huyo alisema maisha yake yameharibiwa na kuwa hana uwezo wa kupata kipato


Security at Tahrir Square, home to the 2011 mass demonstrations that toppled former longtime President Hosni Mubarak, is closely monitored [Khaled Desouki/AFP]


Kisha alijimwagia kimiminika chenye uwezo wa kushika moto na kuwaambia maafisa wa usalama uwanja wa Tahrir kuwa wasimkaribie.


Alisema nchi imekuwa ikiharibiwa vibaya na kundi dogo la “wezi”.


Mtu huyo alijiwasha moto na kisha alipambana na maafisa wa usalama ambao waliuzima moto huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad