Akaunti za Tiffah, Nillan Zasoma Mil. 500



KWA maana kila mwenye nacho ataongezewa! Maneno hayo ya kwenye Kitabu cha Mathayo katika Biblia yanaakisi maisha halisi ya watoto wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Latifah Nasibu ‘Tiffah Dangote’ na Nillan Nasibu ‘Prince Nillan’ kutokana na mkwanja walionao, Gazeti la IJUMAA limedokezwa mchapo kamili.


 


Habari za ndani kutoka kwenye vyanzo makini na vya kuaminika zinaeleza kuwa, kwa pamoja, madogo hao kutoka familia ya wazazi mastaa, Diamond au Mondi na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, wana mkwanja unaokadiriwa kuwa si chini ya shilingi milioni 500 za Kitanzania kwenye akaunti zao za benki.


 


TUJIUNGE NA CHANZO


Akizungumza na Gazeti la IJUMAA kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, mmoja wa watu wa karibu wa Mondi alisema, suala la watoto hao kuwa na mkwanja mrefu siyo ishu kwani wanaogelea kwenye bwawa la utajiri tangu wazaliwe.


“Aaah Tiffah na Nillan tena! Hawa watoto wana pesa jamani, yaani kwa harakaharaka ukiangalia mkwanja wao uliopo kwenye akaunti zao si chini ya shilingi milioni 500. Haiwezi kuwa chini ya hapo tena unasipoangalia unaweza kukuta hata zaidi ya hapo,” kinasema chanzo hicho cha ndani.


 


WAO NI BATA TU…


Mtu huyo alisema kuwa, watoto hao hawazijui shida tangu wazaliwe kwa sababu wazazi wao wamewatengenezea mfumo wa kuingiza pesa.


“Hawataki kabisa watoto wao waje wapate shida hapo baadaye. Si unajua tena mwili wetu lakini pumzi ya Mungu? Hivyo muda wowote wanajua wanaweza kuondoka duniani, sasa wanawaza watawaachaje watoto wao?


“Ndiyo maana kila kukicha wanajitahidi kuhakikisha wanawatengenezea maisha bora ya hapo baadaye ikiwa ni pamoja kuhakikisha wanawatunzia pesa zinazotokana na madili yao.


 


MKWANJA UNATOKANA NA NINI?


“Wana madili ya ubalozi wa kampuni au mashirika ya maana ambayo haya kimsingi ndiyo yanayowafanya wawe na kiasi kikubwa cha pesa kwenye akaunti zao, achilia mbali zile ambazo wazazi kama wazazi wanawawekea watoto wao kwa manufaa yao ya baadaye,” anasema mtu huyo wa karibu.


 


MCHANGANUO ZAIDI


Kwa mujibu wa mtu huyo wa karibu, Tiffah alianza kulamba madili makubwa ya ubalozi tangu pale alipozaliwa ambapo kwa sasa ana umri wa miaka mitano.


Kama ilivyo kwa Tiffah, Nillan naye alipata ubalozi tangu alipozaliwa na sasa tayari ana umri wa miaka minne na mkwanja wa ubalozi umekuwa ukitupiwa kwenye akaunti yake ya benki.


 


“Sasa wewe jaribu kupiga hesabu kwa mkwanja ambao kampuni na benki kubwa yamempa ubalozi Tiffah halafu piga kwa miaka yote mitano, utaona ni mamilioni ya pesa, halafu mpigie pia Nillan kwa miaka minne, si pesa za kitoto,” anasema mtu huyo.


 


WAZAZI NDIYO WANASAINI


Mtu huyo anasema kuwa, pesa hizo ambazo kimsingi wazazi ndiyo wameingia mikataba kwa niaba ya watoto wao, wamekuwa wakiwatunzia mpaka pale watakapokuwa na uelewa mzuri wa kuzitumia.


 


UBALOZI WENYEWE


Gazeti la IJUMAA linafahamu kwamba, Tiffah ni Balozi wa Benki ya NMB, Kampuni ya Vodacom, GSM Mall na Cherish by Carita Adams; kampuni inayodili na fasheni na mitindo ya mavazi iliyopo nchini Afrika Kusini huku mdogo wake, Nillan akiwa ni balozi pia wa GSM Mall.


 


ANACHOKIAMINI ZARI


Kupitia video zake mbalimbali ambazo Zari alijirekodi na kuzungumzia watoto wake hao, anakiri kwamba, Tiffah ana pesa na ndiyo maana anaishi maisha ya kifahari.


“Hao wanaomsema mwanangu kila siku wanataka nini? Mara ooh utasikia sijui kumlea mwanangu, mara sijui ninamvalisha nini, jamani haya ndiyo maisha yake, msitake Tiffah aishi maisha ya kimaskini kama watoto wenu, mwanangu ni tajiri na ana pesa ndiyo maana anaishi maisha haya,” Zari aliwaambia baadhi ya mashabiki mtandaoni ambao hupenda kuingilia maisha ya wanaye.


 


KWA NINI WAMEONGEZEWA?


Tiffah na Nillan ni kama wameongezewa tu utajiri kwani wamezaliwa kwenye familia ambayo baba na mama wapo vizuri kipesa. Mondi amefanikiwa vilivyo kwa kujiingizia mkwanja mrefu kupitia muziki wa Bongo Fleva ndani na nje ya Tanzania.


Mondi anatengeneza mamilioni ya pesa kupitia shoo za ndani na nje ya nchi ambapo kwa shoo moja nje ya nchi, anatajwa kuchikichia si chini ya shilingi milioni 100.


Mondi ana ubalozi wa makampuni kibao, anamiliki kituo cha redio na televisheni, ana nyumba kibao mjini, achana na hayo magari ya kifahari anayotembelea.


 


ZARI SASA…


Kwa upande wake Zari, kule Sauz anamiliki maduka makubwa pamoja na vyuo. Anamiliki nyumba na magari kama yote ya kifahari hivyo watoto hawa ni kama wameongezewa tu utajiri kwani wazazi wao tayari walikuwa wanajimudu kitambo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad