Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomas Simba, ameahirisha kesi inayomkabili Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA,Tundu Lissu na wenzake ya kuchapisha habari ya uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti kwa kile alichokieleza kuwa anaimani tarehe nyingine
Hakimu Simba amesema kuwa kama mshtakiwa atashindwa kufika Mahakamani hapo tarehe iliyopangwa basi hatua nyingine na kisheria zitafuatwa na kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 3 mwaka huu.
Mbali na Lissu, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya jinai namba 208/2016 ni Mhariri wa Gazeti la Mawio, Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh.
Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.
Inadaiwa Januari 12 hadi 14, 2016 jijini Dar es Salaam, washtakiwa Jabir, Mkina na Lissu, waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar.’
Katika shtaka la pili wanadaiwa Januari 14, 2016 walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.