RAIS wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, huenda akafunguliwa mashtaka ya jinai baada ya kukaidi amri ya mahakama kurejea kusikiliza ushahidi wa kesi iliyokuwa inamkabili.
Jaji anayeongoza kwenye kusikiliza shauri la rushwa dhidi yake amesema kuna uwezekano kiongozi huyo akafunguliwa mashtaka ya jinai baada ya kukaidi amri ya kurejea mahakamani kusikiliza ushahidi dhidi yake.
Zuma na mawakili wake waligoma kurejea mahakamani baada ya ombi lao la kutaka kuondolewa kwa Naibu Jaji Mkuu, Raymond Zondo, kwa madai ya kuwa na upendeleo kugonga mwamba.
Mashahidi 34 wanadaiwa kumtaja Zuma kwenye makosa ya rushwa ingawa mwenyewe ameendelea kupinga madai hayo.
Tangu kushtakiwa kwa mara kwanza, Zuma alitumia njia zote za kisheria zinazowezekana kujaribu kufutilia mbali kesi hiyo, bila mafanikio.