Arsenal yachapwa 3-0 na Aston Villa

EMILIANO Martinez kipa namba moja wa Aston Villa  jana Novemba 8 aliibuka shujaa baada ya kutoka na clean sheet kwenye ushindi wa mabao 3-0  dhidi ya Arsenal,  Uwanja wa Emirates. 

Mabao ya Aston Villa ambayo Mtanzania, Mbwana Samatta alicheza hapo msimu uliopita kabla ya kutolewa kwa mkopo nchini Uturuki yalifungwa na Bukayo Saka aliyejifunga dakika ya 25 na Olle Watkins alifunga mabao mawili dakika ya 72 na 75.


Ushindi huo unaifanya Aston Villa iliyocheza mechi 7 kuwa nafasi ya 6 ikiwa na pointi 15 huku Arsenal iliyocheza mechi 8 ikiwa nafasi ya 11 na pointi 12.


Vinara ni Leicester City wakiwa na pointi 18 baada ya kucheza mechi 8 na mabingwa watetezi Liverpool nafasi ya 3 na pointi 17 zote zimecheza mechi 8.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad