Mbunge wa Jimbo la Kawe, Askofu Josephat Gwajima, amewetaka wakazi wa Kunduchi kuwa na subira wakati serikali inaendelea na uchunguzi juu ya eneo lililopatwa na volcano ya tope.
Akizungumza leo hii, mara baada ya kufikia katika eneo hilo lililokumbwa na tope la Volcano Gwajima amesema yeye kama mbunge atahakikisha analisimamia na kulifutilia suala hilo kwa ukaribu sana huku akishirikiana nao.
“Wataalam wetu wanaendelea kufanya uchunguzi ili wajue hiki ni kitu gani kama ni mabaidliko ya hali ya hewa au mzunguko wa dunia kwa hiyo tuvute subira wakati serikali inataka kujua tatizo hili jina lake linaitwa nini” amesema Gwajima
Aidha Gwajima ameongeza kuwa atahakikisha anaiomba serikali kuweza kufanikisha suala la upatikanaji wa tathmini hukua linafanyika haraka huku akiwaahidi wanakunduchi kuwa yajayo yanfurahisha
“Tuangalie ofisi ya serikali inafanya nini katika jambo hili na mimi ntakuwa nao bega kwa bega hakuna mtu atakaye onewa wala kupata shida kwasababu ya jambo hili niwahakikishieni mimi pamoja na wawakilishi wengine tutakuwa pamoja kuona litakalo tokea Kunduchi poleni kwa jambo hili lakini yajayo yanafurahisha” amesema Gwajima