Aston Villa Wamdai Samatta Mabao 15



IMEFAHAMIKA kuwa, mshambualiaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta anayekipiga kwa mkopo katika Klabu ya Fenerbahce ya Uturuki, anadaiwa mabao 15 na timu yake ya Aston Villa ikiwa anahitaji kurejea kwenye timu hiyo.


Samatta amejiunga na Fenerbahce kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Aston Villa ambayo alijiunga nayo Januari, mwaka huu kwa mkataba wa miaka minne na nusu akitokea KRC Genk ya Ubelgiji.


Kabla ya JUZI Jumamosi kucheza dhidi ya Konyaspor, mshambuliaji huyo alikuwa amecheza mechi tano za Ligi Kuu ya Uturuki na kufanikiwa kufunga mabao mawili.


Akizungumza na Spoti Xtra, baba mzazi wa mshambuliaji huyo, mzee Ally Samatta, alisema mwanawe amepewa masharti na Aston Villa ya kufunga mabao 17 katika kipindi chake cha mkopo wa mwaka mmoja.


“Naongea naye sana lakini siwezi kumuuliza kwa nini siku hizi hafungi mabao kwani aliwahi kuniambia kinachotokea kwake huwa kinatokea kwa kila mchezaji, lakini anaendelea kupambana.


“Amefunga mabao mawili hadi sasa, ni jambo ambalo pengine halimpi furaha kwa sababu Aston Villa wamemtaka afunge mabao 17 katika kipindi chake cha mkopo ili waweze kumrudisha England, hivyo sasa anadaiwa mabao 15, ni yeye mwenyewe aweze kupambana kufanya mambo yawe mazuri,” alisema mzee Samatta.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad