MWENYEKITI wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) Taifa, John Pambalu, amesema, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walishatoa msimamo kuhusu uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020, kutokuwa huru na haki lakini wakatokea wanawake 19 wakaenda bungeni kuapishwa.
Pambalu amesema: “Ziko adhabu nyingi za kuchukuliwa kwa hao 19, ikiwa ni pamoja na kuvuliwa nyadhifa zao, kunyang’anywa uanachama. Dhambi ya usaliti ni dhambi mbaya. Hatutaki kushinikiza kamati kuu ichukue hatua gani lakini hatua kali zichukuliwe ikiwemo kuwafukuza uanachama.”
“Bila kujali nafasi zao au wamefanya nini kwenye chama, lazima hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa kitendo hiki. Sababu taasisi hazijengwi na uwepo wa rasilimali tu bali nidhamu pia.”
VIDEO: