BAWACHA "Kina Halima si chochote wacha waende"




Viongozi wa BAWACHA, kutoka mikoa mbalimbali nchini wamekutana kuzungumza, ambapo kwa umoja wao wamelaani vikali kitendo kilichofanywa na wanachama 19 wa chama hicho kwenda kula kiapo cha ubunge bila ridhaa ya chama na kupongeza maamuzi yaliyotolewa ya kuwafukuza uanachama.



Akizungumza hii leo Novemba 28, 2020, Makamu Mwenyekiti wa BAWACHA Zanzibar, Sharifa Suleimani, amesema kuwa licha ya kwamba maamuzi yaliyofanywa na wanawake wenzao wakiongozwa na aliyekuwa mwenyekiti wa baraza hilo Halima Mdee, kiliwahuzunisha sana lakini wao wataendelea kusonga mbele.



"Ninaunga mkono maamuzi ya kamati kuu ya kuwavua uanachama, kutoka hivi sasa wanawake wote tunatakiwa turudi majimboni mwetu, kuendelea kufanya kazi za chama, kuondoka kwao siyo lolote si chochote wacha waende", amesema Sharifa.



Kwa upande wake Mweka hazina wa baraza hilo Catherine Ruge amesema kuwa wanawake wengi walio CHADEMA walimuamini sana Halima Mdee, lakini kawaangusha kwa maamuzi yake, "Wanawake wengi wa CHADEMA tulimuamini Mwenyekiti wetu Halima Mdee, ambaye amefukuzwa uanachama na tulimuona kama mwanamke wa mfano, kiongozi shupavu, jasiri, mwenye msimamo na anayejitambua, lakini Novemba 24,  aliamua kuibadilisha historia yake heshima aliyoijenga kupitia chadema kwa zaidi ya miaka 15 imefutika kwa kweli tunasikitika sana".


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad