Biden, Harris watowa hotuba ya shukurani kwa ushindi uchaguzi wa Marekani



Rais mteule wa Marekani Joe Biden na makamu wake, Kamala Harris, kutoka chama cha Democrat wametowa hotuba zao za kwanza za shukrani kufuatia ushindi wao kwenye uchaguzi uliokuwa na mchuano mkali. 

Akizungumza kwenye uwanja wa Wilmington katika jimbo lake la Delaware, Biden aliwaambia maelfu ya wafuasi wake kwamba Wamarekani wamewapa yeye na Kamala Harris ushindi wa wazi ambao watautumia kurejesha kile alichokiita "roho ya Marekani."


Kwenye hotuba yake hiyo ya shukurani, Biden aliahidi kwamba atakuwa rais wa kuwaunganisha na sio kuwagawa, katika kile kinachoonekana kuupiga kijembe utawala wa mtangulizi wake, Donald Trump, ambaye kauli yake ya "Marekani Kwanza" inatajwa kuleta migawanyiko mikubwa ndani na nje ya Marekani. 


Akizungumza moja kwa moja na wapigakura wenye asili ya Afrika, ambao pamoja na Waislamu walimpigia kura kwa wingi kwenye uchaguzi huo uliokuwa na mchuano mkali, Biden aliwaambia daima wamekuwa wakimuunga mkono kama naye anavyowaunga mkono. 


Kwa upande wake, makamu wa rais mteule, Kamala Harris, ambaye anakuwa mwanamke wa kwanza na pia Mmarekani wa kwanza mwenye asili za Afrika na Asia Kusini kushikilia nafasi hiyo nchini Marekani, alitumia hotuba yake ya shukurani kuwashukuru maelfu ya wanawake wa Kiafrika waliothibitisha kwamba "wao ndio uti wa mgongo wa demokrasia" ya Marekani. 


Kamala, ambaye ni mtoto wa wahamiaji kutokea Jamaica na India, alisema kwamba amepata fursa hiyo ikiwa ni miaka 100 tangu Mabadiliko ya 19 ya Katiba ya Marekani na miaka 55 tangu kusainiwa kwa Sheria ya Upigaji Kura, ambayo iliruhusu idadi ya Wamarekani wenye haki ya kuchaguwa na kuchaguliwa

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad