RAIS mteule wa Marekani, Joe Biden, amesema hatua ya Rais Donald Trump kutokubali kushindwa katika uchaguzi wa urais wa wiki iliyopita ni “aibu” huku akisisitiza kwamba hakuna kitu kitakachozuia uhamisho wa madaraka.
Huku hayo yakijiri Trump amemfukuza kazi Waziri wa Ulinzi, Mark Esper, na kutangaza kwenye mtandao wa Twitter kwamba afisa huyo wa ngazi ya juu wa Marekani “amefukuzwa kazi”. Hii ni baada ya wawili hao kutofautiana hadharani katika wiki za hivi karibuni.
Kitendo hicho kimetafsriwa kuwa Trump ana mpango wa kuivuruga Demokrasi ya Marekani katika kipindi hicho ambacho bado yupo madarakani
Ehhhhh, mbona kazi..!!!
ReplyDeletehuyu mwingine amesha kwea Pipa.
Sijui ana nyumba ya kuweza kukaribisha
wenzake toka mataifa mbali mbali..!!!
Si ukubali uamuzi wa watu, mjenge Taifa.