Bobi Wine akamatwa, IGP afunguka sababu za kumkamata



Kiongozi wa chama cha National Unity Platform (NUP) na mgombea urais wa Uganda, Robert Kyagulanyi, maarufu kwa jina la Bobi Wine amekamatwa mapema leo Polisi nchini Uganda, akiwa katika harakati zake za kufanya kampeni.

Mbunge huyo wa Kyadondo Mashariki, amekamatwa kufuatia mzozo kati ya wafuasi wake na watendaji wa usalama katika eneo lake la kampeni.


Imedaiwa kuwa kukamatwa kwa Bobi Wine, kumekuja baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini humo IGP Martin Okoth Ochola, kumuonya kwamba amekuwa akikaidi miongozo ya uchaguzi yenye nia ya kuzuia kuenea zaidi kwa ugonjwa wa COVID-19.


“Licha ya maonyo yanayotolewa mara kwa mara kwa wagombea, mawakala wao na umma kwa ujumla juu ya athari mbaya na hatari za kiafya za kufanya mikutano na maandamano yasiyoruhusiwa” IGP Ochola


“Tunaendelea kushuhudia vitendo vya kukaidi na kupuuza kabisa miongozo ya EC, kwahivyo wale watakaokaidi miongozo hii ya Tume ya Uchaguzi na mipango yao mibaya inayolenga kuvuruga mchakato wa uchaguzi watawajibishwa” IGP Ochola

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad