POLISI Kanda Maalum ya Dar es Salaam imemkamata Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe, akiwa Kituo cha Polisi Oster Bay jijini Dar es Salaam, alipokwenda kuwaona Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe, na viongozi wenzake wa upinzani wanaoshikiliwa kituoni hapo.
Awali, jeshi hilo lilitangaza kuwasaka wanasiasa Halima Mdee na Zitto Kabwe, huku likiwataka wajisalimishe ili wajibu tuhuma zinazowakabili.
Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Novemba 3, 2020, na Mambosasa imeeleza wanaendelea na oparesheni ya kuwakamata watu wanaofanya mipango kuhamasisha maandamano nchini.
Amesema kuwa hadi sasa jeshi hilo linawashikilia watu 14 wakiwemo viongozi wa Chadema ambao ni Freeman Mbowe, Godbless Lema na Boniface Jacob.
Aidha amesema hali ya jiji la Dar es Salaam imeendelea kuwa shwari, huku akiwataka wanasiasa kuacha kufanya fujo na badala yake kufuata sheria.
Tena ana Damu za Watanzania mikononi.
ReplyDeletePamoja na hao wachache.
Mimi jinsi nilivyo na Hasira nao,labda
muwahifadhi maisha yote, habari itakuwa nyingine. Hawawezi kuwa bora kuliko sisi Mil 60.
Wanataka Waterbord treatment kutoa ubuyu wa wanao watumikisha na sababu.
Haachiwi mtu, na Nondo pia ndani katika mlolongo wa Uhamasishaji mtandaoni kama Ado.