Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa siku mbili kwa wanachama wake 19, ambao jana walikula viapo Bungeni vya kuwa wabunge wa viti maalum bila ridhaa ya chama kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha kamati kuu ya chama hicho kitakachofanyika Novemba 27, 2020.
Kauli hiyo imetolewa leo Novemba 25, 2002, na Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa kwa kuwa jambo hilo ni la dharura wameamua kufuata katiba yao inayosema kuwa, hatua zozote zisichukuliwe bila wahusika kuitwa kujieleza ili kujua ni nini kilichowapelekea wao kukisaliti chama.
"Kwa kuwa jambo hili ni la dharura natangaza wito (Public notice), kupitia vyombo vya habari kwa wanachama wetu 19 walioshiriki kwenda kula kiapo jana, kufika makao makuu ya chama bila kukosa siku ya Ijumaaa ya Novemba 27, 2020, saa 2:00 asubuhi, kutoka popote pale walipo kamati kuu inaweza kuchukua hatua za dharura kama itaona maslahi ya jumla ya chama yanaweza kuathiriwa", amesema John Mnyika.
Aidha Mnyika akizungumzia suala la wabunge hao kula kiapo hicho amesema kuwa, "Mimi kama Katibu Mkuu hakuna fomu yoyote ya mtu yeyote niliyowahi kuijaza popote kuthibitisha uteuzi wa yeyote, hii fomu pia ina sehemu ya kujazwa na kiapo cha hakimu kwahiyo kwa tafsiri nyepesi ni kilichofanyika ni biashara haramu ya kughushi, wameenda kuapishwa bila baraka ya chama".
Wabunge 19 wanaotakiwa kuwasili siku ya ijumaa ni pamoja na Halima Mdee, Ester Bulaya, Esther Matiko na wengine walioapishwa kwa siku ya jana katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.
Hakuna Suala la kuwatisha Kina Mama
ReplyDeleteWabunge Wateule.
Kumbe..!! Hili Povu linaashiria baadhi
ya madai ya kinamama kufanyiwa ile
kama Rushwa ya mchezo wa Kitandani zina ukweli Flani hapa. Wewe Mwanyi kaa kwa lipi la zaidi..?? ujimwambafy
kuita Wabunge wetu bila Adabu na Maadili..?? Jirekebishe na ujue ukomo wako.
Kina Halima,na Wenzake ni Wawakilishi wetu Watanzania na ni Waheshimiwa wanaojiheshimu ukiwahitaji tafadhali jipange hapo 2025 kama watakuwa na muda na wewe na genge lako.
Rushwa ya ule mchezo. SASA BASI.
Kaa Mwinyi kaa, Utawaitaje wabunge wakiwa Jijini Doddoma kwa kipindi hichi ambapo wako katika kazi maalumu za mchakaato wa kibunge.
ReplyDeleteJe mmepitia bunge kuwaita Wabunge..??
Je mnazijua kanuni na vigezo vya kuwaita Wabunge..??
Wacheni ubabaishaji.
HAJI MTU HAPO.