Chanjo nyingine ya COVID-19 yaonesha mafanikio



Kampuni ya dawa ya nchini Marekani iitwayo Moderna imetangaza leo kuwa uchambuzi wa awali unaashiria kwamba chanjo yake inayoendelea kufanyiwa utafiti inaweza kuzuia ugonjwa wa COVID-19 kwa asilimia 94.5. 

Mkuu wa kampuni hiyo Stephen Hoge ameyakaribisha mafanikio yaliyopatikana na kusema yanaleta matumaini kwamba chanjo dhidi ya virusi vya corona itasaidia kuzuia janga hilo na kurejea kwa maisha ya kawaida. 


Matokeo hayo katika hatua muhimu ya majaribio ya maabara yanafanana na yale yaliyofikiwa na kampuni mbili za Pfizer na BioNTech ambazo zilitangaza kwa pamoja wiki iliyopita kuwa chanjo wanayoitengeza imepata mafanikio kwa asilimia 90. 


Umoja wa Ulaya umesema tayari umeanzisha mazungumzo na kampuni ya Moderna ili kupata sherena ya dozi milioni 160 ya chanjo hiyo pindi itapatiwa ithibati.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad