Chanjo ya Corana Kuuzwa kwa bei Nafuu Kwa Nchi Masikini


Shirika la Unicef limetangaza kuhusu mkakati wake wa kusambaza chanjo ya Covid-19 kwa Kenya na nchi nyingine zinazoendelea, limeripoti gazeti la daily Nation nchini Kenya.

Chanjo zote zitakazonunuliwa kupitia Covax zitauzwa kwa shilingi 300 za Kenya (takriban dola 3) kwa nchi zinazoendelea.


Shirika hilo la watoto duniani linasema kuwa limefanya mkataba na zaidi ya ndege 350 na makampuni mengine ya safari za anga kwa ajili ya kusambaza sindano bilioni billion na chanjo.


Takriban sindano milioni 500 za chanjo zitaletwa mwaka ujao. Shirika hilo Jumatatu lilisema kuwa hii itakuwa ni operesheni kubwa na ya haraka ya aina yake kuwahi kufanywa na shirika hilo.


Wataalamu wa Kenya wanatarajia kupokea chanjo za Covid-19 kwa asilimia 20 kwa ajili ya Wakenya. Wahudumu wa afya watakuwa wa kwanza kunufaika kwa kuchanjwa, wakifuatiwa na makundi yaliyomo katika hatari zaidi kama vile wazee.


Likiwa ni mnunuzi mkubwa wa chanjo duniani, Unicef kwa kawaida hununua zaidi ya dozi zaidi ya bilioni mbili kwa mwaka kwa ajili ya chanjo ya kawaida na kwa ajili ya milipuko ya magonjwa kwa niaba ya karibu nusu ya nchi 100.


Jumatatu, Chuo kikuu chaOxford na Astrazeneca pia walitangaza matokeo ya hatua ya tatu ya uchunguzi wa chanjo zao. Hii ndio chanjo ambayo inafanyiwa majaribio katika eneo la Kilifi, lakini matokeo yaliyotangazwa hayajumuishi data kutoka Kenya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad