Chanjo ya kwanza ya virusi vya corona ambayo inaweza inaweza kuzuia zaidi ya asilimia 90 ya watu kupata Covid-19, utafiti wa awali umebaini.
Coronavirus: German company BioNTech says its vaccine is 90% effective | News | DW | 09.11.2020
Wavumbuzi – Pfizer na BioNTech -wanaelezea kuwa ni siku nzuri kwa wanasayansi na kila mtu.
Chanjo yao imewafanyia jaribio watu 43,500 kutoka nchi sita na hakuna wasiwasi wa usalama wao ulioibuka.
Makampuni yamepanga kuomba ruhusa ya dharura ya kutumia chanjo hiyo ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.
Chanjo hiyo inaonekana kuwa tiba nzuri, na inaonekana kuwa njia sahihi ya kukabiliana na marufuku zilizowekwa dhidi ya corona na maisha kurejea kuwa kama kawaida.
Kuna hatua kadhaa za kumaliza jaribio hilo – hatua inayojulikana kuwa jaribio la tatu – lakini jaribio hili ni la kwanza kuonyesha matokeo ya namna hiyo.
Jaribio hili limetumia sindano na vina vya virusi ili kuuweka sawa mfumo wa kinga .
Majaribio ya awali yanaonesha kuwa chanjo inaweza kuweka sawa kinga za mwili -na mfumo mwingine wa kinga ya seli katika kukabiliana na virusi vya corona.
Dozi mbili, ndani ya wiki tatu ndio inahitajika.
Majaribio hayo yamefanyika Marekani, Ujerumani, Brazil, Argentina, Afrika Kusini na Uturuki -inaonyesha kuwa ina kinga kwa 90% ndani ya siku saba baada ya kupata dozi ya pili.
Pfizer inaamini kuwa inaweza kutoa dozi milioni 50 mwishoni mwa mwaka huu, na bilioni 1.3 mwishoni mwa mwaka 2021.
Ingawa kuna changamoto za kitakwimu , kwa kuwa chanjo hiyo inahitajika kuhifadhiwa kwa kiwango cha ubaridi wa 80C.
Kuna maswali kuhusu chanjo hiyo inaweza kudumu kwa muda gani na kampuni hazijaweza kuwasilisha jinsi chanjo hiyo inavyoweza kufanya kazi kulingana na umri pia tofautofauti.
Dkt Albert Bourla, mwenyekiti wa Pfizer,alisema: “Tuko kwenye hatua nzuri ya kuwezesha watu duniani kote kukabiliana na janga la kiafya ambalo limewakumba.”
Prof Ugur Sahin, ambaye ni miongoni mwa waaasisi wa BioNTech, ameelezea chanjo hiyo kuwa ni matokeo yaliyopiga hatua kubwa sana”.
Data zinaeleza kuwa huu sio utafiti wa mwisho.
Hii imejumuisha watu 94 waliojitolea kupima corona -na ufanisi halisi wa chanjo unaweza kubadilika wakati matokeo kamili yatakapo hakikiwa.
Kampuni hizo zimesema zitawasilisha data kamili wiki ya tatu ya mwezi Novemba ili kuipeleka chanjo yao kwa wasimamizi.
Mpaka sasa , si rahisi kwa nchi kuanza kufanya kampeni za chanjo.
Uingereza tayari imeweka oda ya dozi milioni 30.