MUIGIZAJI maarufu wa Bongo Movies, MC Zipompapompa amefariki dunia jana Jumanne, Novemba 10, 2020 nyumbani kwake baada ya kuugua kwa siku chache.
Wakizungumza na Global TV Online, ndugu na marafiki wa karibu wa MC Zipompapompa wameeleza masikitoiko yao kutokana na msiba huo ambao umekuwa wa ghafla sana kufuatia kuugua kwa siku chache.
“Alikuwa anapumua kwa tabu, tukaenda kupima homa, malaria, UTI vyote alikuwa hana, tukapima presha tukakuta ana 160. Waumishi wa Mungu walikuja wakampa maombi na kumuongoza sala ya toba.
“Usiku majira ya saa nane akazifdwa akawa anapata tabu kupumua, nikamchukua ili kumpeleka hospitali; bahati mbaya akawa amefariki hapo nje kabla hatujaondoka kwenda hospitali,” amesema Lona, ambaye ni mtoto wa dada yake Zipompa