Daftari la wapiga kura Uganda lapelekwa Uholanzi kuhakikiwa

 


Gazeti la Daily Monitor la Uganda linaripoti kuwa daftari la kitaifa la wapiga kura limepelekwa Uholanzi kwa ajili ya kuhakikiwa.



Tume ya uchaguzi imeipa zabuni kampuni ya Uholanzi kuondoa majina ya watu walioandikishwa zaidi ya mara moja wakati nchi hiyo ikielekea kwenye uchaguzi mkuu mwezi Januari.


“Tumeanza mchakato wa kuwathibitisha wapiga kura ili kuhakikisha kuwa wapiga kura wanaostahili tu wanaonekana kwenye daftari na kwamba watapiga kura mara moja,” msemaji wa tume hiyo Paul Bukenya amenukuliwa akisema.


Haijulikani kama vyama vya siasa vilijulishwa kuhusu hatua hiyo.


Raia wa Uganda watapiga kura kuchagua rais na wabunge tarehe 14 mwezi Januari. Wagombea 11- akiwemo Rais Yoweri Museveni- watawania nafasi hiyo ya juu.

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kichwa cha Habari si sahihi, Kina Ushabiki, Waandishi jiongezeni katika
    Taaluma na ubunifu on Neutrality katika
    Kuhabarisha. Kalamu yako inaweza kujenga au Kubomoa. Zingatieni Hilo.

    ReplyDelete
  2. Kichwa cha Habari si sahihi, Kina Ushabiki, Waandishi jiongezeni katika Taaluma na ubunifu on Neutrality katika Kuhabarisha. Kalamu yako inaweza kujenga au Kubomoa.

    Zingatieni Hilo.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad