Daktari ahukumiwa, kosa amefanya upasuaji akiwa amelewa na kusababisha kifo



Daktari wa usingizi au nusu kaputi Mbelgiji alijipata akihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela baada ya mwanamke Muingereza kufa baada ya kufanyiwa upasuaji wa dharura wa uzazi (Caesarean) kimakosa.




Helga Wauters, mwenye umri wa miaka 51, alipigwa marufuku kufanya kazi hiyo tena baada ya mahakama ya Ufaransa kusikiliza kesi yake Alhamisi wiki hii.


Alipatikana na hatia ya mauaji ya kifo cha She was found guilty of manslaughter Xynthia Hawke aliyekuwa na umri wa miaka 28 mwaka 2014.


Wauters alisukuma mirija ya kupumulia ndani ya koo la Bi Hawke badala ya kuiweka katika mirija ya hewa, walisema wachunguzi.


Daktari huyo alikuwa amebugia pombe alipokuwa akifanya upasuaji huo.


Wauters hakukata rufaa ya hukumu ya mahakama. Mume Hawke alisafiri hadi katika mji wa Ufaransa wa Pau kusikiliza hukumu dhidi ya mtu aliyemuua mke wake.


Nini kilichotokea kwa Xynthia Hawke?


Bi Hawke alikuwa amelazwa katika hospitali ya Orthez iliyopo karibu na mji wa Pau mwezi Septemba 2014. Alipewa dawa na Wauters, lakini matatizo yakajitokeza wakati wa kujifungua kwa hiyo alihitaji kufanyiwa upasuaji wa haraka ili kuokoa maisha yake nay a mtoto wake.


Wauters, ambaye ni mraibu wa pombe, alikiri kuwa kweli yeye ni mlevi ambaye huanza siku yake “kila siku ” kwa kubugia pombe aina ya vodka na maji. Pia alisema kuwa alikuwa na glasi ya mvinyo kabla yay a kuitwa arejee hospitalini kwa ajili ya kufanya upasuaji siku hiyo.


Mashahidi walisema kuwa daktari huyo alikuwa ananuka pombe aliporejea hospitalini. Alipopelekwa mahabusu, kiwango cha pombe katika damu yake kilikuwa ni gramu 2.38 kwa kila lita , au sawa na takriban glasi 10 za mvinyo (wine)


Xynthia Hawke's family in court on Thursday

Familia ya Xynthia Hawke ilihudhuria mahakamani kusikiliza kesi

Daktari huyo mwenye umri wa miaka 51 alikuwa amepata kazi chini ya wiki mbili alipoingiza mirija ya usaidizi wa kupumua kimakosa. Pia alidai kuwa alitumia mrija wa hewa ya oksijeni badala ya mashine ya usaidizi wa kupumua (ventilator) katika koo la mgonjwa wake.


Marehemu Bi Hawke, ambaye alikuwa anatoka Somerset nchini Uingereza , aligutuka baada ya upasuaji na kuanza kutapika na kupiga mayowe “inauma “, shahidi alisema.


Nesi mmoja aliiambia mahakama kuwa eneo hilo lilikuwa kama la vita.


Alipata mshituko wa moyo na kufa siku nne baada ya upasuaji, lakini mtoto wake alinusurika na kifo.


Lakini daktari Wauters alikanusha kuhusika peke yake na kifo na akasema wafanyakazi wengine pia wanapaswa kulaumiwa . Alidai mashine ya kupumulia ilikuwa haifanyi kazi wakati ule – lakini wachunguzi waligundua kuwa madai yake hayakuwa ya kweli.


‘Sio daktari ‘

Siku ya Alhamisi, mahakama ilimuamuru alipe garama ya takriban euro milioni1.4 sawa na dola milioni 1.65za hasara aliyoisababishia familia ya Marehemu Bi Hawke.


“Haki imetoa mfano kwa aina hii ya daktari ambaye, machoni pangu, sio daktari ,” mume wake Yannick Balthazar alisema.


Daktari Wauters alihamia Ufaransa baada ya kufutwa kazi katika hospitali ya Ubelgiji kwa kufanya kazi akiwa amelewa chakali.


Kampuni iliyomuajiri haikutazama utambulisho wake au rekodi yake ya nidhamu, kulingana na wachunguzi wa kesi hiyo.


“Ninatambua sasa kwamba uraibu wangu haukuwa unaendana na kazi yangu ,”Bi Wauters alisema awali wakati wa kesi yake, kulingana na shirika la habari la AFP . “Nitajutia kifo hiki maisha yangu yote.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad