Kiwanda cha Dangote kinachozalisha Saruji Mkoani Mtwara kilisimamisha uzalishaji kwa takribani wiki mbili ili kusafisha mashine za Kiwanda
Imeelezwa kuwa, hali hiyo ilisababisha Wafanyabiashara watumie fursa kupandisha bei za Saruji kwa mfuko hali iliyofanya Wananchi walalamike. Bei ya saruji ilipanda hadi kufikia Tsh. 35,000 kwa baadhi ya Mikoa
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa alitembelea Kiwandani hapo ili kujua kinachoendelea. Mwanasheria wa kiwanda hicho, Clagu Chuma ameomba radhi kwa kutotoa taarifa