Dodoma. Mbunge mteule wa Mbeya Mjini (CCM), Dk Tulia Ackson amesema hajachukua fomu ya kuwania uspika wa Bunge la 12 ili apate nafasi ya kuwatumia wananchi waliomchagua.
Badala yake, Dk Tulia ambaye katika Bunge la 11 alikuwa naibu spika, amechukua fomu kuwania tena nafasi hiyo.
Dk Tulia ameeleza hayo leo Jumanne Novemba 3, 2020 mjini Dodoma baada ya kuchukua fomu katika ofisi za CCM makao makuu.
Amesema kutokana na majukumu aliyonayo ya kuwatumikia wananchi kwenye jimbo alijipima na kuona akiwa Spika wa Bunge hatakuwa na nafasi kubwa ya kuwatumika.
“Uamuzi wangu wa kutochukua fomu ya Spika haimaanishi nimeogopa ushindani hapana, tukumbuke kuwa nimeweza kumtoa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Mbeya mjini (Joseph Mbilinyi) hivyo siogopi ushindani.”
“Hizi nafasi ni za utumishi na wakati unajipanga kuchukua fomu unakuwa umepima nafasi zilizopo mbele, mimi niliona nitakuwa na kazi mbili ya Naibu Spika na kuwawakilisha wananchi wangu. Kwa muktadha huo nafasi ya unaibu Spika unanipa nafasi nzuri ya kuwawakilisha wananchi na kuweza kumsaidia vyema atakayechaguliwa kuwa Spika wa Bunge,” amesema Dk Tulia.
Katika Bunge la 11 Dk Tulia alikuwa mbunge baada ya kuteuliwa na Rais lakini safari hii alijitosa jimboni na kuibuka na ushindi
good
ReplyDelete